Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro amezindua mradi wa kuzuia
ukatili wa kijinsia ‘GBV Prevention Project’ unaotekelezwa na Shirika la
lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la
mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na
wanawake na makundi yasiyojiweza.
Uzinduzi
huo umefanyika leo Jumatatu Agosti 14,2017 katika ukumbi wa Diamond
Field Hotel mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki
za wanawake na watoto wakiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya
kiserikali,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa,afisa maendeleo ya
jamii,ustawi wa jamii,afisa utamaduni na dawati la jinsia na watoto.
Akizungumza
wakati wa kuzindua mradio huo,Matiro alilipongeza shirika hilo kwa
kuelekeza nguvu zake katika mapambano dhidhi ya ukatili wa kijinsia
ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii husika kwa kushindwa kutoa
ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wahusika wanapobainika.
“Serikali
inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali,ili
mfanikiwe mnatakiwa mshirikishe wadau kwenye maeneo husika,mmefanya
jambo jema kujitambulisha badala ya kuanza kutekeleza mradi kimya kimya
kama baadhi ya mashirika vile yamekuwa yakifanya hali inayowafanya
washinde kufanikiwa”,alieleza Matiro.
“Serikali
ipo nanyi bega kwa bega,pale mnapokwama tafadhali tupeni taarifa nasi
tutawasaidia kadri tutakavyoweza kwani lengo kuu ni kuwahudumia wananchi
wetu ili kuzuia vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa wanawake na watoto
katika jamii”,aliongeza Matiro.
Mkuu
huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuyakumbusha mashirika na taasisi
mbalimbali zinazotekeleza miradi katika jamii kuhakikisha wanashirikiana
na jeshi la jadi ‘sungusungu’,viongozi wa kimila pamoja na watu
mbalimbali wenye ushawishi katika jamii husika.
Akitambulisha
Mradi huo,Mkurugenzi wa TVMC,Mussa Jonas Ngangala alisema mradi huo
unaofadhiliwa na taasisi ya kusaidia asasi zisizokuwa za kiserikali la
The Foundation For Civil Society unaolenga kupiga vita vitendo vya
ukatili wa kijinsia utatekelezwa katika kata tano katika wilaya ya
Shinyanga ambazo ni Usanda,Samuye,Nsalala,Tinde na Didia.
Ngangala
alisema ili kutekeleza mradi huo kikamilifu shirika hilo litashirikiana
na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi serikali,dini,wananchi na wadau
wengine.
“Matarajio
yetu kupitia mradi huu ni kwamba kufikia mwezi Januari mwaka 2018
kuwepo na mfumo mzuri wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kutoka
ngazi ya jamii hadi dawati la jinsia kwa kushirikiana na maafisa
utamaduni,maafisa watendaji,maafisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii
na mashirika mengine”,alieleza Ngangala.
“TVMC
ambayo walengwa wake wakuu ni watoto na wanawake imekuwa ikishirikiana
na serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watoto
wanapata ulinzi na usalama ,elimu na afya bora,msaada wa kisheria kwa
wanawake na watoto lakini pia matunzo kwa watoto”,alieleza Ngangala.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud alisema
kupitia mradi huo wataibua mijadala kuhusu vitendo vya ukatili wa
kijinsia kupitia matamasha,michezo,ngoma za asili,kutoa elimu na mbinu
zingine kadha wa kadha. Katika hatua nyingine Daud alisema ili
kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni pamoja na maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi mkoani Shinyanga ni vyema wadau wote wakashiriki katika
mapambano hayo badala ya kuiachia serikali pekee.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi
wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Shirika la
lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC).
Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud,kushoto ni
Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza ukumbini.
Wadau wa haki za watoto na wanawake wakiwa ukumbini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mkurugenzi
wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized
Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi wa kuzuia
ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika hilo.
wadau wakiandika dondoo muhimu.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi huo.
Wadau mbalimbali walioshiriki katika uzinduzi wa mradi huo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi wa TVMC ,Mussa Jonas Ngangala akisisitiza jambo ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akielezea kuhusu mbinu mbalimbali watazozitumia katika kufanikisha mradi huo.
Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Kiongozi
wa dawati la Jinsia na watoto Shinyanga,Vivian Zabron akichangia hoja
wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia.
Wadau wakiwa ukumbini.
Afisa Utamaduni wilaya ya Shinyanga,Janeth Elias akichangia hoja ukumbini.
Wadau wakiwa ukumbini. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment