Baraza
la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limejipanga kuanza
kutekeleza kwa vitendo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mradi mkubwa
Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleni Tanga kwa
kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi watakaotaka kuzitumia
fursa hizo.
Mradi
huo mkubwa uliosainiwa mwezi mei mwaka huu na kuwekwa jiwe la msingi
hivi karibu na Rais John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda unalenga
kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania.
Katibu
Mtendaji wa Baraza hilo, Bi Beng’i Issa alisema hayo wakati akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwisho mwa juma, kwamba
wamejipanga kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi kuzitumia
fursa za ujenzi wa maradi huo kuanzisha shughuli za kiuchumi.
“Tuejipanga
vizuri katika kuwaelimisha, kuwaonesha fursa zitakazo kuwepo na kuwapa
uwezesha kupitia mifukoa ya uwezeshaji 19,” serikai imeweka fedha katia
mifuko hii hivyo waahitajika kuchagamikia,aliongeza kusema Bi. Issa.
Alisema
ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutoa fursa za ajira 10,000 na baada ya
hapo kutakuwa na ajira 1,000 kwa watanzania, na pia amezitaka Taasisi
za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA kuendelea kuandaa
vijana watakao endana na fursa za ujenzi huo.
Bi.
Issa alizitaja shughuli za kiuchumi zinatarajiwa kuwepo katika mradi
huo ni biashara za usafirishaji wa bidhaa na watu, ujenzi wa miundombinu
mbalimbali, huduma za chakula, uuzaji wa bidhaa za chakula, ulinzi,
uuzaji wa vifaa vya ujenzi.
Zingine
ni huduma zingine ni kama vile afya, sheria, fedha, bima, huduma za
taka, huduma ukarabati na vifaa vya usalama kazini.
Alifafanua
kwamba baraza litashirikiana na mikoa ambayo bomba hili linapita kama
vile Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga
na wilaya 24 na vijiji 184 ili kuhakikisha kwamba wananchi wana shiriki
kikamilifu katika mradi huo.
“Sisi
tumejipanga na tutakuwa karibu na ujenzi huu na fursa zote kadiri
zitakavyo zinajitoeza tutazitangaza katika tovuti yetu “ na pia
watazipata katika halmashauri zao,” alisema
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance
PLC, Bw. James Washima alisema kwamba taasisi yake imejipanga
kuwawezesha watanzania kupata uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali na
wafanya biashara ili kuweza kuzitumia fursa katika mradi huo mkubwa.
“Tunatoa
mikopo ya aia mbalimbali tunawakaribisha kuja kuomba mikopo ili
wazitumie fursa za mradi huu wa bomba la mafuta,” alisema Bw. Washima.
Aliogeza
kusema wanaotaka ni vyema kuwa katika vikundi, watapata mikopo
wanayotaka ikiwemo ya vitendea kazi na mikopo ya kutekeleza zabuni
walizoshida na afuzo ya ujasiriamali.
Naye
Msajili Msaidizi wa Maendeleo na Tafiti wa Bodi ya Usajili wa
Makandarasi (CRB),Bw. David Jere alisema kwamba wakandarasi wanahitajika
kujiunga katika ubia ili kuwa na sifa ya kuingia katika mradi huo
mkubwa wa ujenzi wa bomba hilo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dkt.
John Jingu wa pili kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa
akizungumzia namna baraza litakavyo waelimisha wananchi kutumia fursa za
mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani
Tanga Tanzania, wa pili kulia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i
Issa, kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na
Mikopo-UTT Microfinance PLC. (Picha na Mpigapicha Wetu).
SHARE
No comments:
Post a Comment