Mkuu
wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi (katikati) akizungumza na
washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa na
Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakati alipofungua mafunzo hayo kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kutoka Kamati ya
Olimpiki Tanzania(TOC) Ndg.Suleiman Jabir akizungumza na washiriki wa
mafunzo hayo kutoka mkoani Simiyu (hawapo pichani) ambayo yanafanyikwa
kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.
Afisa
Michezo wa Mkoa wa Simiyu,Ndg.Addo Komba (kushoto) akizungumza katika
mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa maafisa michezo, viongozi
wa vyama vya michezo na walimu wa michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya
Olimpiki Tanzania(TOC).
Baadhi
ya washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa
na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi,
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(hayupo pichani) wakati
akifungua mafunzo hayo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony
Mtaka mjini Bariadi.
Mkuu
wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(wa tatu kulia walioketi)
katika picha ya pamoja na maafisa michezo, viongozi wa vyama vya michezo
na walimu wa michezo wa Mkoa wa Simiyu, wanaoshiriki wa Mafunzo ya
Utawala na Uongozi wa Michezo mjini Bariadi ambayo yameandaliwa na
Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC); (wa pili kulia) Mkurugenzi Mkuu wa
Mafunzo Ndg.Suleiman Jabir
Mkurugenzi
Mkuu wa Mafunzo ya Ndg.Suleiman Jabir Utawala na Uongozi wa Michezo
kutoka Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC)(kulia) akimkaribisha Mkuu wa
Wilaya ya Itilima, mhe.Benson Kilangi ambaye amefungua mafunzo hayo
mjini Bariadi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, MheAnthony Mtaka.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Kamati
ya Olimpiki Tanzania(TOC) imeanza kutoa mafunzo ya siku tano ya Utawala
na Uongozi wa Michezo Mkoani Simiyu, ambayo yamelenga kuleta tija
katika kusimamia na kuendeleza Michezo.
Mafunzo
hayo yanawahusisha Maafisa Michezo Mkoa na Wilaya, Viongozi wa Vyama
mbalimbali vya Michezo na walimu wa michezo kutoka katika baadhi ya
shule za msingi na sekondari mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mafunzo hayo Ndg.Suleiman Jabir amesema lengo kuu la mafunzo
hayo ni kuwasaidia Maafisa Michezo, viongozi wa vyama vya michezo ngazi
ya mkoa na wilaya sambamba na walimu wa michezo kupata mafunzo ya
kiufundi katika kusimamia na kuendeleza michezo, ambayo hutolewa katika
mikoa yote hapa nchini, chini ya usimamizi wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania(TOC).
Akizungumzia
ushiriki wa wanawake Ndg. Jabir amesema Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) imehakikisha kuwa wanawake wanashiriki kwa asilimia 40 katika
mafunzo hayo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati ya Olimpiki ya
Kimataifa la mwaka 2016 la kuwashirikisha wanawake katika masuala muhimu
ya kimichezo ikiwemo suala la uongozi.
Akifungua
mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka,
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi amesema, Utawala na
uongozi wa michezo ulio bora ni msingi wa kuongoza na kuendeleza michezo
kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu.
“Kamati
ya Olimpiki imeandaa mafunzo haya kwa wakati muafaka kwa sababu
wanahitajika viongozi wenye taaluma ya kisasa ya namna ya kuongoza
michezo na wanamichezo,ambao watakwenda na wakati kutenda kazi zao bila
mgongano au vurugu “ amesema Kilangi.
Kilangi
amewataka washiriki kuhakikisha kuwa wanazingatia mafunzo watakayopata
na kuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao, ili mafunzo hayo yasiishie tu
katika Taasisi walizopo bali elimu hiyo ifike hadi ngazi ya vijiji
ambako ndiko kwenye wachezaji wengi.
Aidha,
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa wito kwa washiriki kutumia mafunzo hayo kama
chachu katika kufuata taratibu zote za uendeshaji wa vilabu na vyama
vya michezo katika mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na kufuata katiba.
Ameongeza
kuwa pamoja na kuchukulia michezo kama burudani na sehemu ya kuimarisha
afya, washiriki hao wanapaswa kuwasaidia wachezaji kutumia michezo kama
ajira inayoweza kuwaingizia kipato.
Kwa
upande wake Afisa Michezo wa Mkoa, Ndg.Anthony Komba amesema mafunzo
hayo yatawasaidia washiriki kusimamia michezo kwa weledi mkubwa, kuibua
vipaji na pia yatasaidia vyama vya michezo kusimamia vema vyama vyao,
ikiwa ni pamoja na kufuata katiba hali itakayowasaidia kuepuka migogoro
katika vyama.
Mafunzo
kwa Maafisa Michezo, viongozi wa vyama vya michezo Mkoa na Wilaya
pamoja na walimu wa michezo kutoka katika baadhi ya shule za msingi na
sekondari Mkoani Simiyu, yanafanyika katika ukumbi wa BARIDECO mjini
Bariadi na yatahitimishwa siku ya Ijumaa tarehe 18/08/2017.
SHARE
No comments:
Post a Comment