Kumekua
na vijembe vya hapa na pale kati ya pande mbili za Bongofleva, Diamond
Platnumz na WCB na Alikiba na Rock Star ambapo ishu imeanzia kwenye
fresh remix ya Fid Q ft. Diamond na Rayvanny.
Alikiba
alijibu kupitia ukurasa wake wa Twitter na Instagram ambapo saa kadhaa
baadae kuna kipisi kingine cha hiyo ngoma ya Fresh kilipostiwa Instagram
na Diamond alisikika akichana maneno yafuatayo hapa chini.
“Kufanya verse moja tu naona povu linawashuka, kina dada wavaa top na vibukta.. hawatoi ngoma kazi Twitter kunisuta”
Mistari
hiyo ilisemekana kumdiss Alikiba na Dimpoz ambapo Ommy Dimpoz leo
ametumia ukurasa wake wa Instagram kupost picha akiwa na Mama mzazi wa
Diamond Platnumz na kuandika “BARUA YA WAZI KWA BINTI YANGU MALKIA WA NGUVU, Salam zako nimezipata mwanangu”
“Hivi
kweli ww wa kukosa Adabu na kuamua kunichamba mimi Baba yako? Sasa kosa
langu mimi nini? Kwani kuna Ubaya kumtandikia Kitanda Baby wako King?”
SHARE








No comments:
Post a Comment