Msanii
wa muziki Singeli, Dulla Makabila na msanii wa filamu Bongo Husna
Sajent mapenzi yao wamepamba moto kiasi kwamba kuweka wazi kufunga ndoa.
Dulla
amesema mapenzi yao yalianza miezi saba iliyopita ila hawakutaka kuweka
hadharani ila kwa sasa kwa vile wanaishi pamoja na kila mmoja
amemridhia mwenzake wameamua kuweka wazi.
Ameongeza kuwa yupo tayari kuwalea watoto wawili wa Husna na ni jambo ambalo familia inalitambua.
“Ni
kweli kwa sababu wahenga hawajaacha kitu wanakuambia ukipenda boga
unapenda na ua lake, nashukuru watoto wananipenda na mimi nawapenda na
ninaweza kuwahudumia, familia zimeridhia ndio maana tupo wote,”
ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.
“Tunaishi
tunaheshimiana, huwezi ukaamini tangu niishi na Husna kama aliniboa
sijui kama inafika hata mara tano. Muda mwingi sana tumekaa pamoja,
hatukuchua muda mrefu tukaanza kusihi wote, tulikaa kama miezi miwili,
alikuja home akanogewa basi akasahau kwake, hivyo yaani,” amesema Dulla
Makabila.
SHARE








No comments:
Post a Comment