Rais wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino, ametuma salamu za pongezi kwa
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia kwa
kuchaguliwa kuwa Rais wa TFF kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya
2017-2021.
Rais Infantino katika barua yake
ya Agosti 14, 2017 aliyoiandika kutoka Zurich, amesema: “Ningependa
kuchukua nafasi hii kukupa pongezi zangu dhati. Nakutakia kila la kheri
katika majukumu yako.”
Rais wa FIFA amesema kwamba hana
shaka na uwezo wa Karia hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa Makamu wa Rais wa
kipindi kilichopita, hivyo atakuwa fursa thabiti ya kuiletea nchi
maendeleo ya mchezo soka.
“Kwa wakati wote, nakuhakikishia
ushirikiano wa kutosha kutoka FIFA katika malengo yako. Milango ya FIFA
iko wazi wakati wowote wewe kuja kujadili masuala ya mchezo wa mpira wa
miguu hasa eneo la utawala.
“Ningependa kuchukua nafasi hii
kukualika kuja hapa Zurich wakati wowote kuanzia sasa ambako nitapata
fursa ya kukutambulisha maeneo mbalimbali ya FIFA. Nimeagiza upande wa
utawala kuwasiliana nawe kuona na kupanga tarehe rasmi ya safari,”
amesema na kuongeza:
“Nikutakie tena kheri na fanaka,
nguvu na kila aina ya mafanikio katika majukumu yako mapya huku
nikitarajia ujio wa kuonana nawe haraka.”
Wakati huo huo, Shirikisho la
Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) nalo kwa upande wake wamempongeza
Rais wa TFF, Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa
shirikisho.
Katika barua ya FERWAFA
iliyosainiwa na Rais wa shirikisho hilo, Nzamwita Vincent imesema kwamba
Rwanda itaendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania katika maendeleo ya
mpira wa miguu kwa ushirikiano baina ya nchi mbili kadhalika ukanda wa
Afrika Mashariki unaounda Baraza la Sola la nchi za Afrika Mashariki.
SHARE








No comments:
Post a Comment