TRA

TRA

Friday, August 25, 2017

MANJI KUANZA KUJITETEA AGOSTI 30

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Agosti 25, 2017 imemtia hatiani mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin. Ataanza kujitetea Agosti 30 na 31, mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.
Hakimu Mkeha alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa ana haki ya kujitetea kutokana na mkojo wake kukutwa na dawa aina ya morphine ambayo zao lake ni heroin.
“Hivyo mshtakiwa anapaswa kujitetea kwa sababu Mahakama imemkuta na hatia,”
Baada ya kueleza hayo, Wakili wa utetezi Hudson Ndusyepo alidai kuwa mshtakiwa atajitete kwa hati ya kiapo ambapo watakuwa na mashaidi 15.
Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30 na 31, 2017 na itasikikizwa mfululizo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger