Mchezaji wa ziada
Olivier Giroud alifunga kichwa kizuri katika ushindi wa kushangaza baada
ya Arsenal kutoka nyuma na kuilaza Leicester katika mechi kali ya
ufunguzi wa ligi ya Uingereza.
Alexandre Lacazette aliiweka kifua mbele Arsenal sekunde 94 baada ya kuanzishwa kabla ya Shinji Okazaki kusawazisha dakika mbili baadaye.
Vardy baadaye aliwaweka mbele wageni hao kufuatia krosi muruwa iliopigwa na Albrighton, kabla ya Danny Welbeck kusawazisha dakika za lala salama katika kipindi cha kwanza.
Leicester ilichukua tena uongozi baada ya Vardy kufunga kona iliopigwa na Mahrez hatua iliomlazimu Wenger kufanya mabadiliko yaliozaa matunda.
Mchezaji wa ziada Ramsey alifunga akiwa karibu na goli kutoka kona iliopigwa na Mesut Ozil kabla ya Giroud kufunga kichwa kingine kupitia kona iliopigwa na Granit Xhaka.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment