Mtaalam kutoka Kampuni Tanzu ya
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya GASCO inayojihusisha
na usambazaji wa gesi, Mhandisi Mwanaidi Rashid (kulia) akielezea hatua
iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo Namba I cha gesi ambapo Kiwanda cha
Saruji cha Dangote kitaunganishwa na huduma hiyo kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kutoka
kulia mbele) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa
Ghasia ( wa nne kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na
kamati hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akimpokea
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo (kushoto) aliyeambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Bajeti mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akielezea
mafanikio na changamoto za kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Bajeti (hawapo pichani). Wengine kutoka kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya
Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, akifuatilia
maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa
Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani ) katika kikao
hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (mbele) akielezea
jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao kabla ya
kuanza ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Sehemu ya wajumbe kutoka Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti na watendaji wa kiwanda cha Dangote
wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa unatolewa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (hayupo pichani)
katika kikao hicho.
Kutoka kulia mbele mtaalam kutoka
Idara ya Nishati, Mhandisi Edson Ngabo, Mchumi kutoka Idara ya Sera na
Mipango, Josephat Mbwambo na Kaimu Mkurugenzi kutoka Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge katika kikao hicho.
Mchumi kutoka Idara ya Sera na
Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Josephat Mbwambo (kulia)
akinukuu hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kikao hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji
Mstaafu Josephat Mackanja akifafanua jambo katika kikao hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment