Kwa namna nyingi, Rais Donald Trump wa Marekani na
kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jung-Un wanaweza kuwa tafauti, lakini
ukweli ni kuwa pia kuna mengi wanayoweza kufanana.
Kim Jong-Un ameendelea kusimamia suala la kufyatua makombora
yanayovuuka mabara kwa mara ya pili na kumuweka Donald Trump kwenye
migogoro. Lakini wakati Pyongyang imeshaweka vitisho vya kutumia mabomu
ya nyuklia, safari hii Rais wa Marekani amejinadi kuwa silaha zake
zimefungwa na kujaa na kuahidi kuwa kutawaka moto wenye hasira na
ghadhabu katika kiwango ambacho dunia haijapata kuona.Akizungumza na Gavana wa Guam kwa njia za simu, Trump alisema, "Tunaenda kufanya kazi kubwa hapa, msiwe na wasiwasi kwa chochote. Walitakiwa wawe na mtu kama mimi miaka minane iliyopita, mtu mwenze mawazo mchakato na ule ulikuwa ni wakati na kusema ukweli, mngeweyza kuyasema hay kwa marais watatu waliopita. Lakini mtaangaliwa. Eddie, mmekuwa maarufu dunia nzima inaizungumzia Guam. Nafikiri hata na utalii utakuwa juu. Ninawapongeza."
Baba yake Kim na mtangulizi wa Kim Jong Il alimtengeneza mtoto wake kushika nafasi yake miaka kadhaa nyuma kabla ya kifo chake mwaka 2011.
Kwa upande wa Trump, yeye amefika Ikulu ya White House kwa kutumia taaluma yake ya masuala ya maendeleo na vipindi vya televisheni, pamoja na umaarufu usiokuwa wa kawaida wakati wa kampeni zake.
Tofauti kati ya umri wa Trump na Kim
Wakati huo huo, Kim aliingia madarakani akiwa ni kijana mwerevu na akaendelea kuwa miongoni mwa viongozi wenye umri mdogo duniani na sasa ameshakaa madarakani kwa miaka kadhaa, huku Trump akiwa ni babu wa miaka 70 na ndio kwanza ameingia kwa mara ya kwanza katika nafasi ya kisiasa maishani mwake.
"Kim ana ujuzi kisiasa kuliko Trump ambaye ana umri zaidi ya mara mbili ya wa kwake," anasema John Delury, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Yonsei mjini Seoul, Korea Kusini. "Pengine Kim anadhani ataendelea kubaki madarakani hata baada ya Trump kuondoka," anasema na kuongeza: "Kwa sababu ni mrithi anayeonekana atadumu kutokana na mfumo wa utawala wa kurithishana ina maana ana muda mrefu kuliko wengine."
Kwa taifa lenye vyombo vya habari vitiifu na vinavyomilikiwa na serikali pekee, huku kukiwa hakuna mitandao za kijamii, Kim Jong-Un hana hofu kuhusu magazeti ya kesho yatasema nini au kujibu kwa kutumia Twitter.
Wanaume wote hawa "wamejijengea uaminifu" anasema Delury na wana uwezo wa kuajiri watu wao wanaoweza kusimamia mfumo na, kwa hivyo, kwa hili Trump na Kim wanafanana.
Propaganda kuhusu Pyongyang zinaibua uwiano kati yao, tabia na hata miandiko. Huko Washington, binti waTrump, Ivanka, ni msaidizi maalum wa rais na mume wake, Jared Kushner ni mshauri wa karibu wa rais, wakati mtoto wa kiume wa Trump, Donald Jr amehusishwa na nafasi ya Urusi katika uchaguzi wa Marekani mwaka jana.
"Siasa za kifamilia zimehalalishwa katika mfumo wa uongozi Korea Kaskazini lakini kwa Marekani zimeonekana mara baada ya Trump kuingia madarakani, jambo ambalo si la kawaida kwa Wamarekani," anasema Delury
Kwa sasa nchi hizo mbili zimejifunga katika uwanja wa vitisho wakati ambapo Pyongyang ikitangaza mpango wake wa kutuma makombora katika kisiwa kinachomilikiwa na Marekani katika Bahari ya Pasifiki cha Guam, na Washington nayo ikijibu vikali mashambulizi ya maneno.
"Inaonekana wote wawili wanavitaka vita hivyo. Nadhani wote wananufaika navyo," anasema John Delury, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Yonsei mjini Seoul, Korea Kusini.
SHARE
No comments:
Post a Comment