Mwenyekiti
wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya
Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe.
Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti.Profesa
Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo
Buguruni.
Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake.
"Maalim
analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu
anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni
boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi
hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia
simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni
huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa
kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze"
alisisitiza Lipumba
Aidha
Lipumba amesema kama Katibu Mkuu wa CUF hatakuja ofisini kwa ajili ya
majadiliano na mazungumzo kwa lengo la kumaliza migogoro yao basi Naibu
Katibu Mkuu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba yao ya
CUF.
"Katibu
Mkuu akishindwa kutekeleza majukumu yake Naibu Katibu Mkuu anafanya kazi
kwa kufuata maelekezo ya Mwenyekiti ataendelea Kukaimu nafasi hiyo
mpaka pale Katibu Mkuu atakapokuwa tayari kuja hapa ataruhusiwa kufanya
kazi na ofisi yake ipo hapa, akiwa anakuja ofsini anafuata utaratibu na
kufuata maelekezo yangu mimi sina shida ila kama hatakuja basi Naibu
Katibu Mkuu ataendelea kufanya kazi" alisema Lipumba
Mbali na
hilo Lipumba amesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
toka kimempokea Mhe. Edward Lowassa wameacha ajenda ya ufisadi na
wameiweka kando ajenda hiyo na kusema sasa hivi wao ndiyo ajenda yao
hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment