Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake
Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu Edward Lowassa wametoa pongezi kwa
Rais Mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuongoza nchi
ya Kenya kwa awamu ya pili.
Mbowe amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kuweza kufanya uchaguzi wa uwazi na haki
"Kwa
niaba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na wapenda
Demokrasia wa Tanzania, natoa pongezi kwa chama cha Jubilee na Uhuru
Kenyatta kwa kuchaguliwa tena kuiongoza nchi ya Kenya.Lakini pia
nawapongeza zaidi wananchi wa Kenya kwa uchaguzi wa uwazi na haki, Mungu
ibariki Jumuiya ya Afrika Mashariki" alisema Mbowe
Aidha
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Mhe, Edward Lowassa pia amempa neno
Rais Mteule wa Kenya na kusema kuwa ushindi huo wa pili wa Uhuru
Kenyatta ni kwamba wananchi wa Kenya wamezungumza kupitia kura kuwa wana
imani na uongozi wake na maono yake katika nchi hiyo.
Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilikuwa kinamuunga mkono Rais
Uhuru Kenyatta katika kampeni mbalimbali na kiliweka wazi uhusiano huo
kwa kile kilichodai kuwa Uhuru Kenyatta ni mtu ambaye anasimamia
Demokrasia.
SHARE
No comments:
Post a Comment