Katika kasi ya kuhakikisha madini
ya watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za
madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana
na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda
nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.
Sakata hilo liliibuka baada ya Mh.
Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo
Wilayani Kalambo mpakani na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia
Ziwa Tanganyika.
Usafirishaji wa madini hayo
umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi
wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini
Bujumbura, ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa
wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.
Wakati Mh. Zelote akiendelea na
ukaguzi katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement
ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu
mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya
Mbeya Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.
“Sisi tunajuwa kwamba bandari hii
inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, Haiwezekani
tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials”
kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza
suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na
sio “raw materilas.” Mh. Zelote alisema.
Na kuongeza kuwa Utaratibu uliopo
ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio
utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa
kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe.
Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo
tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za
usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.
Kwa upande wake afisa wa bandari
hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji
wa madini hayo kuwa na mashaka.
SHARE








No comments:
Post a Comment