Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa
wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji
wao huko wenye mitaa yao.
Hawa
ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa
waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta
kabati
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Wenyeviti
wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa
wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi
wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.
Wakizungumza
wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama
cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto
zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.
Wevyeviti
hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na
viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao
unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.
Lakini
wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya
Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na
migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.
“Huku
mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai
ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu
kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu
kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa
kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na
watumishi wa manispaa ya Iringa “walisema wenyeviti
Wenyeviti
hao waliwataka viongozi wa Manispaa ya Iringa kutoa kwa haraka vibari
vya ujenzi maana kumekuwa na ukilitimba mwingi kitu kinachosababisha
ujenzi holela wa makazi kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya
Iringa hivyo viongozi wanapaswa kuwa makini na mikakati madhubuti kwa
kuwa wananchi wanataka kujenga nyumba zao.
Kwa
upande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Sweetbert Maro alisema kuwa kweli posho wanazopewa wenyeviti wa mitaa ni
ndogo hivyo uongozi wa halmashauri ya manispaa imejipanga kukaa pamoja
wenyeviti kujadili jinsi gani ya kuongea posho hizo kulingana na
majukumu wanayoyafanya kuiwakilisha serikali.
“Mnafanya
kazi kubwa mno lakini mnapewa posho kiduchu hivyo tutakaa na kulijadili
hili swala kwa kina kwa kuwa bila wenyeviti wa mitaa halmashauri
haiwezi kupata maendeleo na kukuza mji kwa nguvu zote hivyo tunawaomba
wenyeviti muendelee kufanya kazi wakati swala la posho
linashughulikiwa”alisema Maro
Maro
alisema kuwa atamshauri Mkurugenzi kutafuta muda muafaka wa kukaa
pamoja wenyeviti wote wa mitaa 192 ya halmashauri ya Manispaa ya Iringa
ili kuzijua changamoto na jinsi gani ya kuzitatua maana leo hii mkutano
huu ulikuwa wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.
Aidha
Maro aliwataka wenyeviti wa mitaa kuwabana maafisa watendaji wa mitaa
maana uongozi wa halmashauri umekuwa ukitoa posho kwa wakati kulingana
na agizo la serikali na kufuata sheria ya ugawaji wa posho kwa walinzi
wa amani kwenye mitaa yako.
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa kuna kero nyingine atazipeleka
bungeni ili kuweza kupatiwa ufumbuzi zaidi na kuzitafutia njia za
kuzitatua maana kwa ngazi ya Manispaa wameshindwa kuzitatua.
Kabati
aliwaahidi wenyeviti wote wenye kero za ngazi ya manispaa atahakikisha
zinatatuliwa kwa wakati lakini amewahakikishia kuwa ataitembelea mitaa
yenye kero ambazo zipo kwenye uwezo wake atazitatulia huko huko kwenye
mitaa.
Wenyeviti
hao walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa kuwakutanisha na viongozi wa
halmashauri na kusikiliza kero zao kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi
ambao utaongeza tija ya kuleta maendeleo kwenye mitaa hao.
SHARE








No comments:
Post a Comment