Manchester United imethibitisha kumsajili kwa mara nyingine mshambulizi Zlatan Ibrahimovic.
Zlatan
aliumia na kuamua kuondoka United, lakini imethibitishwa kuwa amerejea
tena Old Trafford na sasa ni shetani mwekundu tena. Wakati wa msimu wa
2016-17, mshambulizi huyo raia wa Sweden aliichezea Man United mechi 46
na kufunga mabao 28 kabla ya kuumia.
Taarifa zinaeleza, safari hii Man United watampa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyehamia Everton.
Hivi karibuni, baada ya kupona, Zlatan alirejea katika viwanja vya mazoezi vya Man United na kuonekana kuwa sasa yuko fiti.
SHARE








No comments:
Post a Comment