Dk Cheni
MWIGIZAJI
wa kitambo Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ amenusa kifo baada ya kupata
ajali mbaya baada ya gari lake kupasuka tairi la mbele na kuparamia
nguzo kisha kupata maumivu makali kwenye bega la mkono wa kushoto.
Kwa
mujibu wa shuhuda wetu, Cheni alikumbwa na mkasa huo usiku wa Alhamisi
iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge, Dar, wakati akitokea Tegeta kwenye
sherehe ya mmoja wa jamaa zake ambapo alipofika eneo hilo, ghafla tairi
la upande wa kulia lilipasuka na kukosa mwelekeo kisha kuivaa nguzo
iliyopo pembeni kabla ya kukwama kwenye jiwe kubwa.
Ijumaa
Wikienda lilipomtafuta Dk Cheni alifunguka: “Dah! Ni kweli nilipofika
pale Bamaga, ghafla nilisikia gari limekuwa zito na hapohapo tairi la
mbele likapasuka. Gari lilikosa mwelekeo nikalielekeza kwenye nguzo,
ninamshukuru Mungu sikupata jeraha kubwa, nimeumia bega la kushoto ila
ninaendelea vizuri,” alisema Dk Cheni.
SHARE
No comments:
Post a Comment