Faustina Charles ‘Nandy’.
MWANADADA
anayefanya poa kwenye Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema
kuwa, hana kitu alichokisahau au kukikumbuka kutoka kwa aliyekuwa mpenzi
wake ambaye pia ni msanii, Billinas.Akipiga stori na Mikito Nusunusu,
Nandy alisema kuwa, licha ya kuwa kwenye uhusiano na msanii huyo kwa
kipindi kirefu na baadaye kumwagana, haoni kitu chochote cha kukumbuka
kwa mwanaume huyo, zaidi ya kuwaza kuongeza juhudi kwenye muziki wake.
Billinas.
“Sina
ninachoweza kukisahau wala kukikumbuka kwa Billinas, kwa sasa sipo naye
karibu kihivyo, namuheshimu kama msanii mwenzangu na si zaidi, muda
ukifika nitamuanika mpenzi wangu wa sasa na kuweka wazi jinsi
anavyonisapoti kwenye kazi zangu,” alisema Nandy.
SHARE
No comments:
Post a Comment