Kiongozi wa
upinzani nchini Kenya, Raila Odinga aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais
uliopita ameliambia gazeti la Financial Times nchini Uingereza kwamba
atafichua ushahidi siku ya Jumanne kuhusu alivyoibiwa kura.
Raila Odinga
Bwana Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
''Sio swala la kuwa mbifansi, Sio swala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena......tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika''.
Bwana Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.
- Kenyatta: Tunakaribisha ushirikiano na wapinzani wetu
- Odinga ayakataa matokeo ya urais Kenya
- Upinzani wadai uvamizi katika afisi yao Kenya
SHARE
No comments:
Post a Comment