Mwenyekiti wa halmashauri ya
Chalinze, Saudi Zikatim akizungumza katika kikao cha mwaka cha baraza la
madiwani la halmashauri hiyo.
Baadhi ya madiwani na watendaji wa
halmashauri ya Chalinze wakimsikiliza mbunge wa jimbo la Chalinze
Ridhiwan Kikwete alipokuwa akizungumza faida na changamoto za hifadhi
zilizopo kwenye vijiji vinavyozunguka hasa Wamimbiki na hifadhi ya taifa
ya Saadan katika kikao cha mwaka cha baraza la madiwani la halmashauri
hiyo
Mbunge wa jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete ,akizungumza kuhusiana na faida na changamoto zilizopo
kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi katika kikao cha mwaka cha baraza
la madiwani la halmashauri hiyo.
Picha na Mwamvua Mwinyi
………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka
madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,kukaa na viongozi wa vijiji
vinavyozunguka hifadhi ya Saadan na Wamimbiki ili kujua mapato
wanayonufaika nayo kwa mwaka na changamoto zilizopo.
Amesema zipo sheria zinazojieleza
kuwa kila kijiji kinachozunguka hifadhi hupata mapato kwa mwaka kama si
mwezi ambapo madiwani na halmashauri hazitambui.
Akizungumza katika kikao cha mwaka
cha baraza la madiwani Chalinze,Ridhiwani alieleza,ipo haja ya kujua
sheria za maliasili zinazosaidia maeneo yao pamoja na kulinda hifadhi
ili kujiongezea kipato.
Aidha alisema kamati ndogo ya
bunge ya mazingira na maliasili iliyoketi hivi karibuni kwa lengo la
kujiuliza juu ya matatizo yanayoendelea kwenye bunga za hifadhi ikiwemo
Wamimbiki inatarajia kufanya kikao na madiwani hao wakati wowote kuanzia
sasa.
Ridhiwani alieleza kwamba,kamati hiyo itakwenda kuzungumza na halmashauri na madiwani hao ili kujua changamoto zinazowakabili .
“Wamimbiki ndio njia kubwa ya
kupita tembo na wanyama wengine wakali kwenda Saadan na ndio njia ya
wanyama wanaotoka Saadan kwenda Ruvuma na Selou”
“Kamati itatakaizungumzie uhifadhi
na kutenga mazingira yetu yakae vizuri na kutengeneza vivutio Wamimbiki
ili tutengeneze fedha nyingi kwa watalii hasa wa picha”alisema
Ridhiwani.
Hata hivyo Ridhiwani alisema,zipo
sheria zinazoruhusu ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri kuwa mwanachama
kwa jambo hilo ambapo pia kila kijiji kinachozunguka hifadhi kwa mwaka
inatakiwa kupata sh milioni.12.
“Kata na vijiji vinavyozunguka
Saadan na Wamimbiki lazima mjue hilo,mie ndio nilijua katika kikao hicho
hivyo fuatilieni kwenye vijiji vyenu mjue kama huwa wakinufaika na
mapato hayo” .
“Unaweza kukuta vijiji havisemi na
wakati mwingine vinahitaji fedha hata za madaftari kwa madiwani.;kama
kweli havijui suala hili basi kikao chetu na kamati ndogo ya bunge
kitasaidia kuleta ufumbuzi wa changamoto zetu”alifafanua Ridhiwani.
Mbali na hayo aliwataka madiwani hao kuendelea kushikamana,kuwa na ushirikiano na kupendana .
Mbunge huyo aliwaomba wachapekazi
kwa kasi waliyoanza nao ili kuiinua halmashauri hiyo ambayo inatoka
kwenye uchanga na kuinua mapato yake zaidi ya sasa.
Nae mwenyekiti wa halmashauri ya
Chalinze,Saidi Zikatim alisema wamepokea taarifa za ujio wa kamati hiyo
kwani itakuwa mwarubaini wa changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Alisema bado kuna kero kubwa ya migogoro ya mipaka baina ya hifadhi na wana vijiji na kusababisha mahusiano yasiyo mazuri.
Zikatimu alibainisha ,hifadhi
zinapaswa kutoa elimu na kutatua changamoto zinazowagusa na jamii ili
kuondoa migongano isiyo ya lazima.
Katika kikao hicho ,diwani wa kata ya Mandela Madaraka Mbonde,alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Katika kikao hicho ,diwani wa kata ya Mandela Madaraka Mbonde,alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti kwa kipindi cha mwaka mmoja.
SHARE
No comments:
Post a Comment