Mkurugenzi wa shughuli za uzalishaji wa viwanda vya TBL Group, John
Gouws,akiwapiga darasa wafanyakazi kuhusiana program hii mpya ambayo
ikitumika ipasavyo itawezesha kupatikana matokeo makubwa.
Meneja wa kiwanda cha Tanzania Breweries Limited (TBL),cha Ilala jijini Dar es Salaam,Calvin Martin,akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa Afya na Usalama wa TBL,Renatus Nyanda, akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wakisikiliza kwa makini jinsi programu hiyo inavyofanya kazi.
…………………………
-Itaongeza ufanisi zaidi kwa viwanda vyake kuelekea Tanzania ya viwanda
Kampuni ya kutengeneza bia Tanzania
ya TBL imezindua programu ya uendeshaji wa shughuli zake kisasa zaidi
na kuwezesha kufanya tathmini ya malengo inayojulikana kitaalamu kama
Voyager Plant Optimization (VPO) lengo likiwa ni kuongeza tija na
ufanisi wa viwanda vya kampuni vilivyopo katika mikoa ya Dar es
Salaam,Mwanza,Mbeya,na Arusha.
Programu hii ya kampuni mama ya TBL Group ya ABINBEV tayari inatumika katika nchi mbalimbali duniani ambako inaendesha biashara zake na imeonekana kuleta mafanikio ya kupima malengo ambayo kampuni imejiwekea na kuhakikisha biashara za kampuni zinaendeshwa katika mfumo unaofanana popote ambapo imewekeza.
Akiongea wakati wa uzinduzi wake
jijini Dar es Salaam,Meneja wa kiwanda cha TBL cha Ilala,Calvin
Martin,alisema kuwa Programu hii mpya inamhusu kila mfanyakazi wa
kampuni kwa kuwa ili mafanikio yapatikane kunahitajika ushirikiano
miongoni mwa wafanyakazi wote na ndio maana kunatolewa mafunzo ya ndani kwa lengo la kumuwezesha kila mfanyakazi wa kampuni kuuelewa vizuri na kuutumia.
Martin alisema kuwa mfumo huu mpya ni endelevu katika shughuli za kila siku za uendeshaji wa viwanda kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uzalishaji sambamba na kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa,kuimarisha usalama maeneo ya kazi na kuzingatia kanuni za utunzaji wa mazingira.
“VPO
itafanikisha kupima ufanikishaji wa malengo tuliyojiwekea ikiwemo
kupunguza gharama za matumizi ya uendeshaji na ikitumika ipasavyo
itaweza kuleta mafanikio ndani ya kampuni kwa kuwa popote ambapo
imetumika imeonyesha kuongeza ubora na ufanisi na kufanikisha malengo ya kampuni ambayo
yako sambamba na malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa
(SDGs) hususani katika maeneo ya utunzaji wa mazingira,matumizi mazuri
ya maji na kuendesha viwanda kwa nishati mbadala zizizo na athari kwa
mazingira”Alisema Martin.
TBL Group kwa kiasi kikubwa imefanikisha malengo mbalimbali ya kupunguza uharibifu wa mazingira ma matumizi mazuri ya maji ambapo kwa upande wa maji matumizi yamepungua kutoka hectolita 6 za
miaka ya karibuni hadi hectolita 3.6 kwa kila lita moja ya bia
inayozalishwa wakati huo mifumo ya utakatishaji wa maji taka ikitumika
lengo likiwa ni ktumia maji kidogo zaidi katika shughuli za uzalishaji
na zisizo za uzalishaji.
Kwa upande wa matumizi ya nishati mbadala rafiki kwa mazingira kampuni
imeanza mkakati za kuzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya jua ambapo
tayari zimeanza kufanya kazi katika kiwanda cha TBL Mbeya na katika
kiwanda cha mwanza tayari kinafanya uzalishaji kwa kutumia sehemu ya
umeme unaozalishwa kutokana na teknolojia ya pumba za mpunga lengo kubwa
likiwa ni kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa,kuzalisha nishati safi na
endelevu vilevile, kupunguza gharama za kununua mafuta.
SHARE
No comments:
Post a Comment