NA WAMJW -ADDIS ABABA – ETHIOPIA
Mawaziri wa Afya Afrika wametakiwa
kutambua kuwa Sekta ya afya ina mahitaji mengi na muhimu kwa nchi
zinazoendelea hivyo hawana budi kuwekeza kwenye vipaumbele vichache
hasa vinavyohusu kuimarisha huduma za Afya ya Mama na Mtoto
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu (Mb)
mbele ya Mawaziri washiriki wa Mkutano wa 4 wa Kuondoa Vikwazo katika
kuokoa Maisha ya Mama na Mtoto.
“Katika mkutano huu ambao umefunguliwa na Mhe. Dkt. Mulatu Teshome, Rais wa Jamhuri ya watu wa Ethiopia unajadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kumaliza vifo vya mama na mtoto, kuongeza usawa katika upatikanaji wa huduma za Afya kwa kuondoa vikwazo, kuboresha ubora wa huduma za afya na kuimarisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango ya utoaji wa huduma za Afya” alisema Waziri Ummy.
“Katika mkutano huu ambao umefunguliwa na Mhe. Dkt. Mulatu Teshome, Rais wa Jamhuri ya watu wa Ethiopia unajadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kumaliza vifo vya mama na mtoto, kuongeza usawa katika upatikanaji wa huduma za Afya kwa kuondoa vikwazo, kuboresha ubora wa huduma za afya na kuimarisha matumizi ya takwimu katika kupanga mipango ya utoaji wa huduma za Afya” alisema Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy alieleza
kwamba mipango mbalimbali na changamoto ambazo Tanzania na nchi nyingi
za Kiafrika zinakabiliwa nazo katika kufikia mipango endelevu ya
upatikanaji wa rasimali fedha katika kutekeleza afua mbambali za sekta
ya Afya.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
katika kukabiliana na changamoto ya Rasilimalifedha alisema Tanzania
inakamilisha mchakato wa kuwa na Bima Moja ya Taifa ya Afya ambapo pia
itaweka sharti kwa kila Mtu kuwa na Bima ya Afya ili kuwezesha wananchi
kuwa na uhakika wa matibabu pindi wanapogua.
Mbali na hayo Waziri Ummy
alisema kuwa Serikali ya Tanzania imeanzisha mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha fedha kidogo zilizopo zinatumika vizuri ikiwemo kutoa fedha
kwa Vituo vya Huduma kulingana na Matokeo/utendaji wao (Result Based
Financing) ambapo vituo vya tiba vilivyokuwa na hali mbaya (nyota
sifuri) vinapewa fedha kuboresha huduma ambapo maboresho makubwa
yameonekana katika vituo hivyo ndani ya kipindi kifupi.
Aidha Waziri Ummy alielezea uamuzi
wa Serikali wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye Vituo badala ya
kupelekwa kwenye Halmashauri (Direct Financing Facility) ambapo
utekelezaji wa mpango huu umeanza tarehe 1 Julai 2017.
Waziri Ummy Mwalimu ameongoza
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Muhimu wa Kimataifa wa kuondoa vikwazo
katika kuokoa maisha ya Mama na mtoto unaofanyika Addis – Ababa,
Ethiopia Agosti 24 hadi 25 mwaka huu katika mjadala alioshiriki w a
kuimarisha upatikanaji endelevu wa rasilimali fedha katika sekta ya
afya.
SHARE
No comments:
Post a Comment