"Ha ha ha Wanawake tunaweza" Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela wakipongezana kwa furaha isiyo kifani na Mkurugenzi wa Amorette Ltd. Mama Jacqueline Mengi wakati wa uzinduzi huo. |
Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika,
Getrude Mongela amesema wakati umefika kwa wanawake kuajiri na kufukuza.
Alitoa kauli hiyo katika sherehe za Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwaendeleza
Wanawake Afrika (WAA) iliyofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini
Dar es Salaam. Jukwaa hilo linasimamiwa na Taasisi ya Graca Machel.
Mama Mongela alikuwa akijibu maswali ya waandishi kuhusiana na hisia
zake baada ya uzinduzi na majadiliano ya Kitabu “Women Creating Wealth”
ambazo ni simulizi la wanawake wajasiriamali katika bara la Afrika,
waliofanikiwa na safari yao katika ujasiriamali.
Alisema ingawa wakati wa Mwalimu Nyerere juhudi zilifanyika kuwawezesha
wanawake, kundi hilo lilibaki kufanyakazi za kufungasha au kushona,
lakini kizazi cha sasa kimeendelea kiasi ya kwamba kina uwezo wa kufanya
uwekezaji na kuwa waajiri. Rais
wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela akifanya mahojiano na
mwandishi wa kituo cha Televisheni cha ITV, Henry Mabumo mara baada ya
uzinduzi wa kitabu cha Kitabu “Women Creating Wealth” wakati wa sherehe
za Uzinduzi wa Jukwaa la Kuwaendeleza Wanawake Afrika (WAA) iliyofanyika
kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo
linasimamiwa na Taasisi ya Graca Machel.(Picha zote na Thebeauty.co.tz)[/caption]
Alisema amefurahishwa sana na maelezo ya ndani ya kitabu hasa safari
mbalimbali za wanawake kuanzia vijana na wale wa kati ambao wamethubutu
na kuonesha njia ya ujasiriamali bila kukata tamaa na hivyo kuwa mfano
kwa wengine.
Alisema katika mahojiano hayo kuwa wanawake kwa sasa wakati umefika wa
kuwa na viwanda vikubwa, kumiliki na kuwezesha mabadiliko ambayo
yatachochea maendeleo binafsi, familia na hata taifa.
Anasema wanawake waliachwa nyuma kutokana na wanaume kutotambua au
kutokubali uwezo wa mwanamke na sasa vijana wanaonesha kwamba wanawake
wanaweza na wanathubutu. Mshereheshaji
wa uzinduzi wa kitabu cha Kitabu “Women Creating Wealth” Mwasisi wa
Re-Write, Chidiogo Akunyili akisherehesha uzinduzi wa kitabu hicho
uliofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam.[/caption]
Pamoja na kazi hizo amesema wakati umefika wa wanawake kutumia akili ili
siku moja kipuri kitengenezwe na mdada na watu wajisikie fahari kwenda
kukitumia.
Akizungumzia kitabu hicho Mwasisi wa mtandao wa She Inspires Her, Lisa
O'Donoghue-Lindy amesema kwamba kinatoa maelezo ya safari ya
wajasiriamali wa kike, dhiki zao, changamoto na namna walivyoanzisha
ujasiriamali wakati mwingine wakiwa na fedha kidogo kiasi cha dola 23
katika mifuko yao.
Alisema kitabu hicho kimeandaliwa kutoka wajasiriamali mbalimbali
takribani 60 wa bara la Afrika kwa lengo la kutoa hamasa kwa
wajasiriamali wengine ambao wanachipukia au wale ambao wanataka
kuthubutu. Muasisi
wa mtandao wa She Inspires Her, Lisa O'Donoghue-Lindy akielezea
yaliyomo kwenye kitabu cha "Women Creating Wealth” ambacho ni simulizi
za wanawake 60 wajasiriamali katika bara la Afrika, waliofanikiwa na
safari yao katika ujasiriamali.[/caption]
Alisema kwamba maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hicho ni binafsi mno,
kwani walizungumzia ubunifu na safari ya kiuchumi waliyoianzisha wadada
hao na namna waliyvoondoka katika changamoto mbalimbali. Aidha kimelenga
kushawishi watoa maamuzi kutoa nafasi ya wanawake kuendelea na kuona
umuhimu wao katika kuimarisha maendeleo na usawa.
Miongoni mwa watu waliomo ndani ya kitabu hicho Jacqueline Mengi,
Esther Karin Mngodo, Devotha Minzi na Mtendaji wa kampuni ya uhandisi ya
Mount Carmel Seline Mwenelupembe. Wapo pia wajasiriamali kutoka Kenya,
Uganda na Kongo ya Kinshasa.
Akizungumza kuhusu kuwamo katika kitabu hicho Jacqueline Mengi alisema
anajisikia furaha kuwa mfano wa kuwafundisha wengine, akisema kwamba
anaona fahari kuwaambia wanawake wenzake kwamba kujiamini ni silaha
muhimu na kwamba ukishinda nafsi ni lazima ufanikiwe. Mtendaji
wa kampuni ya uhandisi ya Mount Carmel Ltd Seline Mwenelupembe ambaye
ni mmoja wa wanawake wajasiriamali waliomo ndani ya kitabu hicho
akielezea safari yake ya ujasiriamali ambapo mpaka sasa ametoa ajira ya
kudumu kwa watu 50 nchini kwake.[/caption]
Aliwataka wanawake kushikamana na kupeana ushirikiano katika safari
hiyo.
Naye Renee Ngamau Mtangazaji wa redio kipindi cha Capital in the Morning
kutoka kampuni ya Capital Group Limited alitoa hongera kwa kukazabuti
kwa washiriki wote waliomo katika kitabu kwamba wamefanyakazi moja
muhimu ya kuonesha wanawake kwamba ujasiri na uthubutu ni kitu cha
muhimu katika kuamua maisha yao binafsi. Alisema wanawake hao wameonesha
kwamba kwa hali yoyote ile mwanamke akifanya maamuzi ya kuendelea mbele
ataweza.
Anasema wanawake ndio msingi mkubwa wa maendeleo kwa kuwa asilimia 90 ya
pato lao hulirejesha katika familia kwa shughuli mbalimbali za kijamii. Mtangazaji
wa redio kipindi cha Capital in the Morning kutoka kampuni ya Capital
Group Limited, Renee Ngamau akitoa pongezi kwa washiriki waliomo katika
kitabu cha “Women Creating Wealth” wakati wa uzinduzi wa kitabu
hicho.[/caption]
Akielezea siri ya mafanikio yake Devotha Minzi ambaye kwa sasa ana
kampuni ya ushauri kuhusu namna ya kuingia katika ujasiriamali, alisema
kwamba mambo ambayo yamekuwa yakimfikirisha sana ni kuhusu namna ya
wahitaji wanavyoweza kupata fedha benki na wala si benki kutoa fedha.
Minzi ambaye aliwahi kuajiriwa Benki Kuu aliacha kazi yake hiyo na
kuingia katika kuwekeza katika taasisi ya fedha kabla ya kuachana nayo
na kuanzisha kampuni ya ushauri.
Akizungumza katika mkutano huo alisema kwamba wakati anaingia katika
ujasiriamali alitambua kwamba kuna shida ya kujiweka sawa kuchukua fedha
za Benki na hivyo kuona haja ya kuwapa elimu wanawake kuhusu Benki
kuwapa fedha na si kunung’unika kwamba hawapewi fedha. Mwanauchumi
Devotha Minzi akielezea siri ya mafanikio yake wakati wa uzinduzi wa
kitabu cha “Women Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca
Machel uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption]
Alisema ni vyema wanawake kufanyakazi zao kwa akili zaidi na kuhakikisha
kwamba wamejiandaa vyema katika kuhakikisha kwamba mahitaji yao
yanatekelezeka kwa kutambua mambo ambayo ni muhimu katika uwekezaji na
kuwa na nguvu.
Anasema mpaka alipofika yeye amekumbana ana changamoto nyingi lakini la
maana ni kuwa ana ratibu na anaangalia zaidi mahitaji na taratibu zake
akiongeza kwamba kwa sasa amejikita kutoa ushauri wa kuwawezesha
wanawake wenzake kukopesheka. Mkurugenzi
wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi na Mtaalamu wa masuala ya fedha na
CEO wa Philips Tanzania, Monica Joseph wakifurahi jambo wakati wa
uzinduzi huo.[/caption]
Alisema ni vyema watu wakabadilika kifikra na kutengeneza utaratibu
ambao utawafanya benki wawape hela bila hata kuombwa.
Katika jukwaa hilo wanawake walipata nafasi pia ya kuhutubiwa na Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye
aliwataka wanawake kusaidia serikali katika kuhakikisha uchumi unakua. Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi na baadhi wanawake wenzake wajasiriamali wakitambulishwa kwenye uzinduzi huo. Mkurugenzi wa Amorette Ltd. Mama Jacqueline Mengi na CEO wa Philips Tanzania, Monica Joseph katika uzinduzi huo. Baadhi
ya wanawake wajasiriamali kati ya 60 kutoka bara la Afrika ambao
simulizi zaoza safari ya ujasiriamali zimo katika kitabu cha “Women
Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca Machel wakiwa
kwenye picha ya pamoja akiwemo Mama Jacqueline Mengi. Muasisi
wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel katika picha ya pamoja na
wanawake wajasiriamali kati ya 60 waliondikwa kwenye kitabu cha “Women
Creating Wealth” kilichoandaliwa na Taasisi ya Graca Machel. Muasisi wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akiwapongeza wakinama hao mara baada ya picha ya pamoja. Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho. Muonekano
wa nje wa Kitabu cha “Women Creating Wealth” ambacho kinasimulizi za
wanawake wajasiriamali katika bara la Afrika, waliofanikiwa na safari
yao katika ujasiriamali akiwemo Mama Jacqueline Mengi. Ukurasa
wa ndani ya kitabu cha “Women Creating Wealth” ambao umechapisha
simulizi za safari ya ujasiriamali ya Mkurugenzi wa Amorette Ltd,
Jacqueline Mengi. Muasisi
wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel akisalimiana na kumpongeza
Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi mara baada ya uzinduzi wa
kitabu cha “Women Creating Wealth” uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela (aliyeipa mgongo kamera)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Amorette Ltd, Jacqueline Mengi
(wa tatu kushoto) Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu (wa pili
kushoto), Mmiliki wa duka la ENJIPAI, Nasreen Kareem (kushoto) wakati wa
hafla ya uzinduzi wa kitabu cha “Women Creating Wealth” uliofanyika
jijini Dar es Salaam. "Ha
ha ha Wanawake tunaweza" Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika, Getrude
Mongela wakipongezana kwa furaha isiyo kifani na Mkurugenzi wa Amorette
Ltd. Mama Jacqueline Mengi wakati wa uzinduzi huo. Mkurugenzi
Mtendaji wa IBRA Construction Limited Bi. Maida Waziri Juma ambaye pia
ni miongoni mwa wanawake 60 walitoa simulizi za kufanikiwa na safari yao
katika ujasiriamali. Muasisi
wa Taasisi ya Graca Machel, Graca Machel katika picha ya pamoja na
Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyalandu mara baada ya uzinduzi wa
kitabu hicho.
SHARE
No comments:
Post a Comment