Na Mahmoud Ahmad Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha
Mrisho Gambo amewaagiza watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya
Arusha kufanya kazi kwa weledi na umoja ili waache alama ambayo
itakumbukwa na wananchi wanaowahudumia.
Gambo aliyasema hayo
mapema jana alipokuwa akizungumza na viongozi,na watumishi wa
halmashauri hiyo ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara siku tano ya
kutembelea miradi na kuongea na wananchi ikiwa ni mwendelezo wa ziara
yake aliyokuwa nayo ya kutembelea halmashauri zote za mkoa wa arusha.
Alisema kuwa watumishi
ni viongozi ambao wamepewa dhamana kubwa ya kuwaongoza wananchi na hivyo
wanapaswa kufanya kazi kwa weledi huku wakihakikisha kuwa wanafuata
kanuni,sheria na taratibu ili waweze kuacha alama ambayo daima wananchi
wataikumbuka pindi watakapoacha utumishi wao.
Vile vile aliwaagiza
maafisa kilimo wa halmashauri hiyo kutoka maofisini na kuhakikisha kuwa
wanaenda kutoa huduma za kitaalamu kwa wanachi walioko vijijini kwani
wapo wakulima wanaolalamika kutoonekana kwa maafisa kilimo hivyo kukosa
utaalamu wa kilimo.
Hata hivyo gambo
amewasihi watumishi wote wanaokabiliwa na changamoto ya kutopanda
madaraja,na malimbikizo ya mishahara waendelee kuchapa kazi na kuwa
wavumilivu kwani serikali inaelewa changamoto hizo na kwamba changamoto
hizo zimetokana na uhakiki wa watumishi pamoja vyeti feki na taratibu
zikishamakizika wataanza kulipwa staiki zao zote.
Awali
mkurugenzi wa halmashauri hiyo dt Wilson Mahera akisoma hotuba yake
alisema kuwa katika halmashauri hiyo wanakabiliwa na changamoto ya
upungufu wa wafanyakazi hivyo kuathiri utoaji huduma kwa wananchi ambapo
changamoto hiyo inatokana na wale wote waliokuwa wakitumia vyeti feki
katika halmashuri hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment