Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda wakisaini
mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika hafla iliyofanyika Dar es
Salaam leo. Wengine wanaoshuhudia ni maofisa kutoka benki ya NMB na
Viguta.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin
Dauda wakibadilishana hati baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid NsekelaAbdulmajid Nsekela
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda.
Taswira meza kuu.
Wanachama wa Viguta wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Viguta.
Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja Wadogo na Wakati wa NMB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Viguta, Eva Mbone.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin Dauda, akizungumza.
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo, Wateja Rejareja, Omari Mtiga akizungumza.
Mada ikitolewa.
Majadiliano yakifanyika.
mkutano ukiendelea.
Wafanyakazi wa NMB wakijadiliana
Meneja Mwandamizi wa Huduma na Amana wa NMB, Stephen Adili akijibu maswali.
Wanakikundi wakiwa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
Zaidi ya
wanachama 100 watanufaika na Ushirikiano baina ya Benki ya NMB na Umoja
wa Vicoba Tanzania (VIGUTA), baada ya kutiliana saini ya mkataba wa
ushirikiano.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kutiliana saini mkataba huo wa ushirikiano jijini
Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ineke Bussemaker
alisema leo ni siku ya kipee kwa benki hiyo kwa kusaini mkabata wa
ushirikiano na Viguta ambao utafungua ukurasa mpya katika sekta ya
kifedha nchini.
Alisema
benki hiyo siku zote imekuwa karibu na wananchi katika utoaji wa huduma
zake na katika ushirikiano huo itatoa mafunzo ya utunzaji wa fedha kwa
wateja wao.
Alisema
huduma watakayoweza kunufaika nayo wanachama ni ile ya akaunti ya pamoja
kupitia vikundi ambapo wanachama wao wataweza kukopa mikopo yenye riba
nafuu na kuweza kujua mambo mbalimbali kama kujua salio kwa kutumia simu
zao za mkononi.
Alisema
benki hiyo imejipanga vizuri kutoa huduma kwa wateja wao pamoja na kutoa
elimu kwa kila mtu na ushirikiano huo utakuwa ni endelevu.
Alisema
wanaounda akaunti ya pamoja ni makundi ya watu kutoka katika familia,
makundi ya wanawake, marafiki na makundi ya whatsApp.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Viguta ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Salmin
Dauda alisema umoja huo una wanachama milioni 7 huku ukiwa na vikundi
92,000 ambao wananufaika na benki hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment