Moja ya gari lililohusika katika ajali hiyo.
……………………………………………………………..
Watu wengine tisa walijeruhiwa
kati yao wanaume ni wanne na wanawake watano. Aidha kati ya majeruhi
hao, wawili wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na saba wamelazwa
Hospitali Teule Ifisi – Mbalizi. Chanzo cha ajali kinachunguzwa hata
hivyo inahisiwa kuwa dereva wa lori alikosa umakini na kuanza kugonga
magari mengine ambaye pia amepoteza maisha katika ajali hiyo. Upelelezi
unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ajali na dereva aliyehusika.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo
mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na
uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na
kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya
linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za
barabarani kwa kuhakikisha madereva na watumiaji wengine wa barabara
wanafuata sheria na alama za usalama Barabarani. Aidha kumekuwa na ajali
01 ya vifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 14.09.2017 majira ya
saa 19:45 usiku huko eneo la Mlima Iwambi, Kata ya Songwe, Tarafa ya
Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya
Mbeya kwenda Tunduma, kulitokea ajali iliyohusisha magari matano yenye
namba za usajili T. 231 BME aina ya Tipper ikiendeshwa na dereva FRED
MWAKALINGA [33] Mkazi wa Itiji – Mbeya ikitokea Mbeya mjini kwenda
Mbalizi, Gari yenye namba za usajili T. 515 ARE aina ya Fuso iliyokuwa
ikiendeshwa na dereva EMMANUEL JULIUS [29] Mkazi wa Itiji ikitokea
Mbalizi kwenda Mbeya mjini, Gari yenye namba za usajili T.126 DJZ aina
ya Fuso basi iliyokuwa ikiendeshwa na AMOS MWAIKAJA @ CHODO [40] Mkazi
wa Kagera – Soweto, Gari yenye namba za usajili BCA 8730 na tela BCA
8733 ikiendeshwa na EVANS MUSONDA [39] raia wa Zambia na Gari yenye
namba za usajili T.570 CKC aina ya Toyota dyana ikiendeshwa na dereva
AMOS BENSON pamoja na Pikipiki moja ambayo haijafahamika namba zake za
usajili ikiendeshwa na dereva aitwaye JANIA JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi
wa Iwambi.
Katika ajali hiyo watu wanne
walifariki dunia ambao ni dereva wa Gari yenye namba za usajili T.570
CKC AMOS BENSON, mwendesha Pikipiki ambayo bado hajafahamika namba zake
za usajili aitwaye JANIA JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi wa Iwambi, dereva wa
Gari lenye namba za usajili BCA 8730/BCA 8733 EVANS MUSONDA [39] raia
wa Zambia na Mwanamke mmoja ambaye bado hajafahamika ambaye alikuwa
abiria kwenye Gari yenye namba za usajili T.570 CKC Toyota Dyana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa Madereva
kuwa makini wanapotumia vyombo ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Aidha Kamanda MPINGA anawataka madereva kufuata, kuheshimu na kuzingatia
sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali.
Imesainiwa na:
[MOHAMMED R. MPINGA – DCP]
SHARE
No comments:
Post a Comment