Mwamuzi wa kimataifa, Elly Sasii
atakuwa mwamuzi katika mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars ya
Tanzania na Zebras ‘Pundamilia’ ya Botswana utakaofanyika kesho Jumamosi
Septemba 2, mwaka huu.
Katika mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam waamuzi
wasaidizi watakuwa Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati
mwamuzi wa akiba (Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.
Mchezo huo utaanza saa 10.00 jioni
unaochezwa chini utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), limepanga Watazamaji waingie uwanjani kwa kiingilio cha Sh 10,000
kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum
Mayanga leo Ijumaa amezungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hosteli ya
TFF, Karume jijini Dar es Salaam ambako amethibitisha kwamba kikosi
chake kiko imara kwa mapambano.
Kwa upande wa Kocha wa Botswana,
David Bright amesema yeye ni kocha mpya na amejitahidi kuteua timu mpya
yenye mchanganyiko wa vijana na wazoefu aliokuja nao kuwajaribu kwa
nyota wa Kitanzania.
Taifa Stars iko kambini na nyota
wake akiwamo Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli
(Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah
(Sony Sugar/Kenya),Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Simon Msuva
(Difaa El Jadidah ya Morocco).
Wengine ambao wako kambini Hoteli
ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula
(Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young
Africans).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael
(Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young
Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao – Nahodha
Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC),
Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young
Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).
SHARE
No comments:
Post a Comment