ZAIDI ya Pikipiki 350 alimaarufu bodaboda zimekamatwa na Jeshi laPolisi Mkoani Tanga kutokana na makosa mbalimbali ya usalama barabarani ikiwemo madereva wake kutokuvaa kofia ngumu pindi watumiaji vyombo hivyo.
Pikipiki
hizo zilikamatwa wakati wa operesheni ya Jeshi hiloinayoendelea katika
maeneo mbalimbali Jijini Tanga ikiwa ni mkakati wa kupambana uvunjifu
wa sheria za usalama barabarani na kupunguza ajali
ambavyo vimekuwa zikigharimu maisha ya wananchi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Benedict Wakulyamba (Pichani Juu}
aliwaambia waandishi wa habari kuwa zoezi la ukamati wa pikipiki
hizo limetokana na ukaidi wa madereva na abiria wa kutokutii sheria
za barabarani ikiwa pamoja kutokuwa na leseni .
Alisema katika ukamataji huo pikipiki 206 ambazo zilikamatwa na madereva
wake wakikabiliwa na makosa ya kutokuwa na kofia ngumu, madereva 87
hawakuwa na leseni,pikipiki 33 hazikuwa na bima 25 mbovu na 5 kuzidisha
abiria(mshikaki).
Aidha alisema kufuatia hali hiyo jeshi hilo baada ya kujiridhisha
na hatua za kisheria pikipiki 244 zilitozwa tozo za papo kwa
pao,32 dereva na abiria wake walifikishwa mahakamani,32 walionywa
kutokana na
utaratibu wa kisheria na 48 bado zipo kituo cha polisi cha mabawa kwa hatua zaidi za kisheria.
“Niseme tu kutii sheria bila shuruti limeonekana kama jambo geni
hasa hapa Jijini kwetu na watu walifikiri ni kitu hakiwezekani
lakini tumeliamua kweli na tutashughulika nao wanaokaidi sheria
za barabarani”Alisema Kamanda Wakulyamba.
Alisema kumekuwepo na malalamiko dhidi ya jeshi hilo kuwa ukamataji
wa pikipiki hizo hauzingatii utaratibu wa kisheria kutokana na namna
ya ukamataji wake unavyofanyika ikiwa pamoja na askari kuvaa kiraia na
hata kuwavizia katika baadhi ya maeneo.
“Hatuwezi kupangiwa jinsi ya kumkamata mtu
tunayemuhisi anamakosa,kinachofanywa na askari wangu ni kumsimamisha
mwendesha boadaboda au chombo chochote cha moto lakini kama hataki
kutii tunalazimika kumkamata kwa njia yoyote”Alisema Wakulyamba.
Hata hivyo amewatahadharisha wananchi Mkoani hapa kuwa zoezi hilo
si nguvu ya soda na litaendelea ikiwa sehemu ya kukomesha virendo
vya kutokutii sheria za barabarani na hakutakuwa na simile kwa atakae
kamatwa awe derva au abiria wote wataingia kwenye makosa.
SHARE
No comments:
Post a Comment