Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi fomu za
kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), na vipeperushi
mbalimbali vyenye taarifa za kina kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo,
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Humphrey
Polepole, wakati alipotembelea banda la Mfuko kwenye maonesho
yaliyoambatana na Tamasha la Jinsia 2017, lililoandaliwa na Mtandao wa
Jinsia Tanzania, (TGNP), kwenye viwanja vya Mtandao huo Mabibo jijini
Dar es Salaam, Septemba 8, 2017.
|
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Humphrey Polepole,(pichani juu),
amefurahishwa na mpango wa uchangiaji wa hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
kutokana na faida azipatazo mwananchama hususan bima ya Afya.
Bw.
Polepole alionyesha kuridhishwa kwake na mpango huo ujulikanao kama PSS, baada ya kupatiwa maelezo kuhusu faida
mbalimbali azipatazo mwanachama, wakati alipotembelea banda la PSPF kwenye
maonesho yaliyoambatana na Tamasha la Jinsia 2017, lililoandaliwa na Mtandao
wa Jinsia Tanzania, (TGNP), kwenye viwanja vya Mtandao huo, Mabibo jijini Dar
es Salaam, Septemba 8, 2017.
“Mpango
huu ni mzuri kwani serikali ya CCM iliwaahidi watanzania kuwapatia huduma ya
afya ambayo itawafikia watanzania wote na mimi ninaamini kwa viwango
mlivyonitajia watanzania wengi wanaweza kumudu kuwa na bima ya afya,”
alifafanua Bw. Polepole.
Alisema
yeye yuko tayari kushirikiana na PSPF katika kuwapatia elimu wana CCM na
wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mpango huo. “Mimi tayari ninayo bima ya
afya, lakini niko tayari kuhamasisha wananchi ili waweze kujiunga na mpango huu
kwani ni mzuri, na kinachohitajika ni elimu kuwafikia ili waelewe umuhimu wake.” Alifafanua Bw.
Polepole.
Akimpatia
maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na PSPF, Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Bw Abdul Njaidi alisema, Mpango wa uchangiaji wa hiari umelenga
makundi mbalimbali ya wananchi wenye shughuli inayowapatia kipato kama vile,
madereva wa bodaboda, mama lishe, machinga na wajasiriamali wengine.
“Kujiunga
na mpango huu ni bure, na mwananchi aliyejiunga na mpango huu atapaswa
kuchangia kiasi cha fedha kisichopungua shilingi elfu 10,000/= kila mwezi,
lakini jambo la muhimu zaidi, pamoja na kufaidi mafao mablimbali, mwanachama
pia atakuwa na fursa ya kujiunga na bima ya afya,” alifafanua Bw. Njaidi.
Naye
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, akifafanua zaidi
alisema, mpango wa PSS umekuwa na faida kubwa kwa wananchi ambao wengi wamekuwa
wakihitaji kupatiwa bima ya afya.
“Muitikio
wa wananchi kujiunga na PSS umekuwa mzuri kwani wengi wao huhitaji kupatiwa
bima ya afya kwa hivyo sisi kama PSPF tunawahamasihsa wananchi kutumia fursa
hii ya kujiunga na PSS kwani ukiacha fao hilo la afya kuna mafao mengine kama
mikopo ya elimu, viwanja na nyumba.” Alifafanua Bw. Delphin.
Kando
na Bw. Polepole kutembelea banda la PSPF, pia Wananchi mbalimbali
waliweza kufika kwenye banda hilo kupatiwa elimu kuhusu shughuli na
huduma zitolewazo na PSPF, miongoni mwa waliofika ni Mkurugenzi Mtendaji
wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, ambaye naye aliahidi kuwaunganisha
wanachama wa Mtandao huo ili waweze kukutana na maafisa wa PSPF
kuwapatia elimu kuhusu umuhimu na faida za kujiunga na PSPF kupitia
Mpango wa uchangiaji wa Hiari.Kongamano hilo lililozinduliwa na Makamu
wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan Septemba 5, 2017, limefikia kilele
Ijumaa Septemba 8, 2017,.
|
Bw. Polepole, (kulia), akimsikilzia kwa makini, Bw. Njaidi.
Afisa
Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto), akitoa
ufafanuzi zaidi kuhusu huduma zitolewazo na PSPF, kupitia Mpango wa
Uchangiaji wa Hiari, kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha
Mapinduzi, Bw. Humphrey Polepole.
Afisa Msaidizi wa PSPF, Bw. Win-God
Mushi, (kulia), akimpatia maelezo, Bi Agness G. Lukanga aliyetembelea
banda la PSPF na kisha kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS)
Afisa Msaidizi wa PSPF, Bw. Win-God Mushi, (kulia), akiwapatia maelezo, waanchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo.
Afisa
Uendeshaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF Bw. Delphin Richard,
(kushoto), akimpatia maeelzo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian
Liundi, alipotembelea banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi.
Bw. Polepole, (kulia), akizungumza mbele
ya Bw. Njaidi ambapo alitoa ushauri mbalimbali na kuahidi kusaidia
kuhamasisha wana CCM na wananchi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa
Hiari PSS.
Mama huyu akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa PSS.
Mama huyu akipigwa picha ya
kitambulisho cha uanachama wa PSPF, kupitia Mpango wa PSS, ambapo
mwanachama hupatiwa kitambulisho punde tu anapojiunga.
|
Mama huyu akipigwa picha ili kupatiwa kitambulisho cha uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa PSS.
|
Bw. Delphin, (kulia), akimpatia vipeperushi vya PSPF mama huyu aiyetembelea banda la Mfuko huo.
Bw. Delphin, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na PSPF, Bi.Agness G. Lukanga.
No comments:
Post a Comment