Tajiri mmoja raia
wa China anayeishia mjini New York ambaye amewalaumu maafisa wa vyeo vya
juu nchini China kwa kuhusika kwenye ufisadi ameomba kupewa hifadhi
nchini Marekani, kwa mujibu wa wakili wake.
China imetaka bwana Gua akamwe lakini mashtaka dhidi yake hayajulikani.
Vyombo vya habari vimamemlaumu tajiri huyo wa umri wa miaka 50 kwa kumpa hongo naibu waziri mmoja, madai ambayo bwana Guo anayakataa.
Bwana Guo ambaye aliondoka China mwaka 2014, amechapisha ujumbe kadha katika mitandao ya twitter na YouTube zinazofichua ufisadi baina ya wanachama wakuu wa chama cha kikomisti cha China.
- Mtu tajiri zaidi barani Asia ziarani Kenya
- Waliohukumiwa kimakosa nchini China walipwa dola milioni 1.3
- Mwanamke tajiri zaidi Afrika atajirika zaidi
- Mwanzilishi wa Amazon sasa ndiye mtu tajiri dunia
- Trump amteua tajiri kuwa balozi Uingereza
Mwezi Aprili serikali ya China ilitoa agazi kwa polisi wa kimqtaifa wa Interpol kutaka Bw. Guo akamatwe.
Mamlaka za China pia zinaripotiwa kumchunguza Bw. Gao kwa takriban uhalifu 19 ukiwemo utekaji nyara na ulanguzi wa pesa.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment