Wapenzi wa
muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka kwa
wasanii nguli kutoka nchi za Afrika kupitia onyesho la Coke Studio linalorushwa
na Clouds TV ambapo mwishoni mwa wiki ‘kolabo’ ya mwanamuziki kutoka nchini, Izzo
Business na Avril kutoka Kenya imeacha gumzo kubwa.
Wanamuziki
wengine waliopagawisha mashabiki wa muziki katika onyesho hilo ni Mafizikolo kutoka Afrika ya Kusini kwa
kushirikiana na msanii Nyashinski kutoka nchini Kenya
na wasanii waalikwa Bill Nas (Tanzania), Sheebab (Uganda) na Asgeg Ashko
(Ethiopia).
Akiongea juu ya
kolabo hii, Izzo Business alisema amefurahi kushirikiana na Avril kimuziki hususani
wimbo walioimba pamoja unaojulikana kama ‘kanyonyi kanja’ na ‘mabata mabata yanaogelea’ ambao umeimbwa kwa lugha ya
Kiswahili ukiwa na vionjo vya muziki wa bongofleva.
Kupitia onyesho
hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca-Cola, muziki wa Tanzania
unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao
wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika. Shindano hili linarushwa kwenye luninga
kwenye nchi zaidi ya 50.
Wasanii wa
Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny,
Izzo Bizness, Nandy na mtayarishaji nguli wa muziki wa studio, Nahreel.
Wakitoa maoni
yao kuhusiana na onyesho hili, baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa
mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni
moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi
mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona
anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live).
Mbali na wasanii
wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka
katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda,
Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire,
Madagascar, Mauritius, Mozambique, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Cameroon.
Baadhi ya
wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya), Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah,
Ykee Benda ( Uganda).
Wengine ni Nasty
C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka
Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa
Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana.
Tangia onyesho
hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika
kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali
za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na
kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
SHARE
No comments:
Post a Comment