Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la
Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani ni Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi
pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe
(kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia)
mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya
mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo
mbali mbali kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale kutoka kwa
Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt. Agness Gidna
mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la
Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia historia
kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale iliyopo kwenye Makumbusho
ya Olduvai mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale
katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia uzinduzi
wa tovuti na mtanzao wa bure wa Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya
kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani
ya hifadhi ya Ngorongoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia mara
baada ya kufungua kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika
bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
…………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi
wanaoishi kwenye bonde la Ngorongoro kuwa mstari wa mbele katika
kuhifadhi na kutunza mazingira ya bonde hilo ili liwe na manufaa kwa
kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Makamu wa Rais aliyasema hayo
leo wakati wa ufunguzi rasmi wa Makumbusho mapya ya Olduvai –
Ngorongoro. Katika ufunguzi huo Makamu wa Rais pia alipata nafasi ya
kuzindua tovuti maalum kuhusu masuala ya utalii katika bonde la
Ngorongoro. “Ufunguzi huu ninaoufanya leo unaendana na malengo
tuliyojiwekea ya kuongeza na kukuza vivutio vya utalii ili kuvutia
wageni (watalii) wengi zaidi kutembelea nchi yetu” alisema Makamu wa
Rais.
Akihutubia mamia ya wananchi
waliojitokeza katika tukio la ufunguzi wa Makumbusho hayo, Mheshimiwa
Makamu wa Rais alisema anatamani kuona kinachofanyika Ngorongoro
kinafanyika pia katika maeneo mengine yenye rasilimali za kihistoria
kama vile mapango ya Amboni (Tanga), Michoro ya Miambani ya Kondoa
(Dodoma), miji mikongwe ya Zanzibar, Bagamoyo, Kilwa Kisiwani na Songo
Mnara.
Pia Mheshimwa Makamu wa Rais
aliwaagiza viongozi wa Serikali, hususani Wizara ya Tawala za Mikoa na
serikali za Mitaa pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kutambua,
kulinda, kuhifadhi na kuendeleza vivutio vyote vya kiutamaduni na
kijiolojia vilivyopo nchini. “Nataka kuona shughuli za kiutalii
zikiibuka katika ngazi ya wilaya kupitia Halmashauri zetu na ofisi za
Wakuu wa Wilaya ili kuongeza ajira za vijana nchini” alisisitiza Makamu
wa Rais.
Makamu wa Rais alitoa rai kwa
wananchi wote wanaoshi pembezoni au karibu na rasilimali za kitamaduni
kutunza rasilimali hizo muhimu kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.
Makamu wa Rais alisema ”ninyi ni mashuhuda wazuri wa namna rasilimali
hizi zilivyo muhimu kwa ustawi wa uchumi wenu, ajira mnazopata, heshima
ya kutambuliwa utamaduni wenu kimataifa pamoja na fedha za kigeni
zinazopatikana kupitia utalii unaotokana na rasilimali hizi ambazo
husaidia kujenga huduma za kijamii kama vile mahospitali, mashule,
barabara na miundombinu ya maji”. Aidha alisisitiza kuwa serikali
haitasita kuchukua hatua kali kwa viongozi wa serikali, wataalam na
wananchi watakaosababisha uharibifu wa rasilimali muhimu kwa
kutotekeleza majukumu yao sawasawa au kuvunja sheria na taratibu za
uhifadhi wa rasilimali hizo.
Mwisho, Makamu wa Rais
aliwashukuru wote waliohusika katika ujenzi wa Makaumbusho hii mpya na
ya kipekee duniani hususan Umoja wa Ulaya ambao wamechangia kiasi
kikubwa cha fedha za kukamilisha ujenzi huo.
Ufunguzi wa Makumbusho ya
Olduvai uliohudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne
Maghembe(MB), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo, Naibu Waziri wa
Kilimo na Mifugo Mhe. Ole Nasha (MB), Balozi wa Umoja wa Ulaya na
Balozi wa Hispania pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.
SHARE
No comments:
Post a Comment