Kampuni ya StarTimes
Tanzania inayouza King’amuzi cha StraTimes, imetangaza kuwa, imepata
haki ya kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani
nchini Urusi.
Hayo yamesemwa na
Meneja wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Gasper Ngowi, katika hafla
ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo huadhimishwa kila wiki
ya kwanza ya mwezi Oktoba.
“Tunapenda
kuwataarifu wateja wetu kuwa king’amuzi chetu cha StarTimes kimepata
haki za kuonyesha michuano ya Kombe la Dunia ambayo itafanyika mwakani
nchini Urusi, hivyo ni wakati wao sasa kuchangamkia fursa hiyo kwa
kulipia ving’amuzi vyao,” alisema Ngowi.
Naye Mkurugenzi na
Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luo, amesema: “Katika
kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, tumekuja na kitu kipya ambapo
tumeongeza chaneli kwenye king’amuzi chetu kwa ajili ya kuwapa burudani
zaidi wateja wetu kwani tunawajali sana.”
Pia Luo amesema ili
kuwafikia wateja wao kwa haraka na kuwatatulia matatizo yao, katika
kitengo chao cha huduma kwa wateja wameongeza watu na kufikia 300 ambapo
wateja wao watakuwa wakiwasiliana nao kwa namba 0764700800 na
0677700800.
SHARE
No comments:
Post a Comment