Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo.
Mkuu
wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi
(katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa
promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.
Kampuni
ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake
inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja
wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za
fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya
SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure.
Akiongea
wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo
wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la
promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote
zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza,
Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa.
“Kampuni
yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga
mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta
furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya
‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote
inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi
mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY
LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi.
Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua.
Iambatanisho
laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu
kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya
shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja,
ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni
kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda –
kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele.
Kisusi
aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na
soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo
kama zilizvyo zawadi kubwa. “Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia
promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na
kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha
na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.”
Kuhusu
jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa
bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala
maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye
kiwanda cha Nyanza Bottlers. Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo
zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite,
Tangawizi, Sparleta na Novida.
SHARE
No comments:
Post a Comment