Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' , akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' , akionesha
kompyuta mpakato kwa wanahabari ambayo alianza kuitumia baada ya
kuanzisha blogu hiyo miaka mitatu iliyopita.
Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi,
William Malecela 'Le Mutuz' (kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, kuhusu blogu hiyo kutimiza miaka mitatu na
semina itakayowakutanisha wasomi wasio na kazi kuhusu namna ya kujiajiri
badala ya kutegemea kuajiriwa.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Blogu ya Wananchi Media kesho
itaadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, sherehe itakayofanyi
Hyatt Regency Kempisky zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar
es Salaam leo, Mkurugenzi wa blogu hiyo, Wiliam Malecela (Le Mutuz),
alisema kuwa wameamua kufanya sherehe kutokana na mafanikio waliyopata
katika kipindi hicho, bendi ya muziki wa kizazi kipya ya THT
itatumbuiza.
Alisema licha ya kesho kufanya sherehe ,
leo itakuwa na semina maalumu ya vijana 300, ambao watakuwa pamoja na
matajiri 6 vijana na vijana watatu viongozi wa wa kitaifa kwa lengo la
kubadilishana mawazo na matajiri na viongozi hao, ambao wataeleza
walivyopigana mpaka kufikia walipo kimaisha.
Alisema alianzisha blogu hiyo baada ya
kuisajili kwa msajili wa makampuni (Brela) 2012, ikianza kwa kutembelewa
na watu 200 kwa siku lakini kwa sasa inatembelewa na watu 70,000 mpaka
100,000 kwa siku kitu ambacho anajivunia na kuwashukuru wadau.
Kampuni hiyo ilianza kwa mtaji wa dola
ya Marekani 500, ikiwa na usajili wa makampuni wa Brela, na inatoa ajira
kwa vijana 4 waliomaliza vyuo vikuu nchini na ina ofisi yake katika
jengo la Tancot House Sokoine Drive, Dar es Salaam.
Alisema katika miaka mitatu blogu
imeweza kuwa na domain yake wenyewe ya www.williammalecela.com na
kuingia kwenyeFacebook, Twitter, na Instagram ambapo sasa inarushahabari
sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja na kuweza kuwafikia watu hadi
500,000 kwa siku.
Alisema mipango ya baadaye ni kuwekeza
kwenye kampuni mpya ya African Swahili Media Radio & Television
ambayo tayari imeshapata leseni ya kufungua radio na televisheni ambayo
inatazamiwa kuwa hewani Aprili mwaka huu, kituo cha radio kitakuwa
Morogoro na televisheni Dar es Salaam, anatarajia kutoa ajira zaidi
angalau kwa vijana 10.
SHARE
No comments:
Post a Comment