![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa sisitiza jambo wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC). |

Mkurugenzi
Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es salaam
wakati alipotangaza mpango mpya wa shirika hilo ambapo linaanza kuuza
nyumba kwa wafanyakazi wa Mashiriki Binafsi na wachangiaji Binafsi
waliojiunga katika mifuko ya jamii ambapo amesema tayari utaratibu huo
umeshaanza na mtu yeyote ambaye ni mwanachama katika mifuko ya Jamii na
ni mtumishi wa Serikali au mashirika binafsi au mchangiaji binafsi
anaruhusiwa kununua nyumba katika shirika hilo kama mnununzi mpangaji wa
shirika hilo na baada ya miaka 25 akimaliza deni lake au akimaliza
kabla ya muda huo atakabidhiwa hati ya umiliki wa nyumba hiyo na kuwa
mmiliki kamili, Katika Picha kushoto ni Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC)

Mkurugenzi
Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akimsikiliza
Bw. Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC) wakati
alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo
kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC)

Mkurugenzi
Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa akieleza
jambo katika mkutano huo kwa jinsi shirika hilo lilivyojizatiti katika
uuzaji wa nyumba zinazojengwa katika miradi yake hapa nchini , kulia ni
Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC) na kushoto ni Bw.
Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo (WHC)

Mkurugenzi
Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa na Bw.
Raphael Mwabuponde Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo
(WHC)wakimsikiliza Irene Kasanda Afisa Mauzo wa (WHC) wakati akielezea
namna wana Diaspora wanavyoweza kunufaika na mpango huo.

Mkurugenzi
Mkuu wa Watumishi Housing Limited (WHC) Dk. Freddy Msemwa sisitiza
jambo wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa
habari kulia ni Maryjane Makawia Afisa Mauzo na Mwasiliano (WHC).
………………………………………………………………………..
Watumishi
Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja ulio anzishwa kwa
lengo la kujenga na kuuza nyumba za bei nafuu kwa Watumishi wa umma kwa
mikopo nafuu ya muda mrefu.
Watumishi
Housing Company (WHC) inapenda kuijulisha umma kwamba imefungua dirisha
kwaajili ya kuuza nyumba zake kwa wafanyakazi wote. Hii inajumuisha
wafanyakazi walio katika utumishi wa umma na wale ambao hawako katika
utumishi wa umma lakini wanachangia katika mifuko ya pensheni. Wigo huu
mdogo unakuja baada ya kuonekana watu wengi ukitoa watumishi wa umma
wana shida ya makazi bora na ya kisasa ni wachangiaji katika mifuko ya
pensheni ambayo ndiyo wamiliki wa Watumishi Housing, hivyo basi taasisi
ikaona itoe nafasi kwa wachangiaji wengine wa mifuko ya pensheni kuweza
kupata nyumba za kisasa, bora na za bei nafuu.
Kufuatia
uamuzi huu, Watumish Hosing Company sasa itakua ikiwahudumia watumishi
wa umma pamoja na wafanyakazi wengine walioko katika sekta binafsi.
Uamuzi huu ni muendelezo wa juhudi za serikali na mifuko ya hifadhi ya
jamii katika kuwawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora na
kuwawezesha kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba.
Watumishi
Housing inapenda kuwakaribisha watanzania wote kwa ujumla kutuma maombi
yao ya nyumba kwa kuchukua fomu katika tovuti ya www.whctz.org au
kwa kufika katika ofisi zilipo jengo la Golden Jubilee Towers ghorofa
ya 4. Kwasasa tuna nyumba za kuuza zilizopo Bunju B, Gezaulole
Kigamboni, Mkundi Morogoro, Mwanza Kisesa na Njedengwa Dodoma. Vilevile
tunapenda kusisitiza kwamba watumishi wa umma watapewa kipaumbele katika
kupata nyumba kwani wao ndio kipaumbele cha taasisi.
Watumishi
Housing Company (WHC) ni mfuko wa uwekezaji wa pamoja wenye jukumu la
kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi wa umma. Jukumu
lingine la WHC ni kusimamia dhamana ya uwekezaji nyumba (Real estate
investment Trust- REIT) kupitia uwekezaji katika vipande. WHC
inamilikiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii lakini baada ya muda si mrefu
WHC itaweza kumilikiwa na kila mtanzania kupitia uwekezaji wa vipande.
Watumishi
Housing tunashauri watumishi kununua nyumba tayari zilizojengwa na
zilizo bora na za kisasa badala ya kununua ardhi na kuanza ujenzi.
Kwakufanya hivi utakua unanunua nyumba ambayo tayari imeishajengwa kwa
ubora na kisasa kwa bei nafuu kabisa vilevile utakua unaondokana na
matatizo mengi sana yanayokuja na ujenzi kama kupoteza muda, gharama
kubwa
SHARE
No comments:
Post a Comment