




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
KAMPUNI
ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom imekabidhi kwa shule ya
sekondari ya Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini, msaada wa mashine
yenye uwezo wa kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurufu karatasi.
Msaada
wa mashine hiyo (Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni
sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi
wa “Pamoja na Vodacom” imekabidhi shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato
30.
Mbali
na msaada wa Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu
kutoka shirika lisilo la kiserikali la Learning in Sync kwa ajili ya
kuweka program maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia .
Mkuu
wa Vodacom Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa
mashine hiyo ni muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa
Pamoja na Vodacom imeendelea kutoa kwa nchi nzima.
“Huu
ni muendelezo wa msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha
sehemu ya faida kwa wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia
wadogo zetu kuingia katika digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na
maisha ya baadae,”alisema Tzamburakis.
Alisema
Mashine hiyo ya kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa
zikiikabili shule hiyo hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na
machapisho mengine ambayo shule ili lazimika kuingia gharama kubwa
kuchapisha.
Katika
kuhakikisha walimu wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo
Tzamburakis alisema ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu
kwa ajili ya kufundisha namna ya kuitumia.
“Ofisi
ya kanda ya Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa
mafunzo kwa walimu ya namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka
utaratibu wa kufika mara moja kwa mwezi katika shule hii ili waweze
kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo hayo.”alisema Tzamburakis.
Kwa
upande wake mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe, Jacob Costantine
aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo huku akieleza changamoto
zilizoikabili shule hiyo ikiwemo ya kuchapisha mitihani kwa gharama
kubwa .
“Tumepewa
mashine ya Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada
ya kumueleza kuwa tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha
mitihani ,kuchapisha mitihani yetu ya mihula na ile ya mwisho wa
mwaka”alisema Costantine.
Alisema
kupatikana kwa mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa
kuchapisha machapisho mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji
wake umekuwa mgumu kwa ajili ya wanafunzi hao kujifunzia.
Mkuu
huyo wa shule alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne
kwa ajili ya maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha
ya kuandika ubaoni mitihani ya majaribio itatoweka.
SHARE
No comments:
Post a Comment