Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana
jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii,
Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya
NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla
Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la
Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double
Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi
wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za
kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na
Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na
Huduma kwa Jamii cha NHC.
Waziri
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wilfred Lwakatare akiongozana na
Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina
Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa
nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda
na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina
Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge
ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC
Mwongozo.
Naibu wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula na
Mkurugenzi wa nyumba kutoka Wizara wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Michael Mwalukasa wakijadiliana jambo katika ziara hiyo
Wajumbe
wa Kamati hiyo wakiongozana na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Mikoa, Raymond Mndolwa wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara
katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment