Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri vilabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, timu za Azam FC, JKU na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
Katika
salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri timu hizo kuhakikisha
zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika
hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na
watanzania wote.
Timu ya
JKU ya visiwani Zanzibara leo Ijumaa watakua kibaruani kuchuana na SC
Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Amani mjini
Zanzibar.
Kesho
Jumamosi, Yanga SC watakua wenyeji wa APR ya kutoka nchini Rwanda katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa
na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini
Shelisheli.
Jumapili
Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika
Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa
Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na
Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka
Sudan Kusini
SHARE
No comments:
Post a Comment