TRA

TRA

Wednesday, March 16, 2016

Man City yatinga robo fainali klabu bingwa Ulaya, matokeo kamili yapo hapa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


3204
Klabu ya Manchester City  usiku wa kuamkia leo wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 3-0, baada ya mchezo wao uliopigwa katika dimba la Etihad, kumalizika kwa sare ya 0-0 dhidi ya wapinzani wao Daynamo Kyiv.
Matokeo hayo ya sare ya bila kufungana yalitegemewa kwa hamu kubwa na mashabiki wa klabu hiyo ya Manchester City ilikuweza kusonga mbele kwenye michuano hiyo na hadi kipyenga cha mwisho matokeo yalibaki 0-0.
Mchezo wa awali City ilifanikiwa kutoa kichapo kwa Dynamo Kyiv cha mabao 3-1, hivyo katika mchezo wao huo usikuu huu unawafanya kutinga hatua hiyo ya robo fainali kwa jumla ya pointi nne na mabao 3-1.
Kwa upande wa mchezo mwingine kati ya Atletico Madrid na PSV hadi kipyenga cha mwisho timu hizo zilitoka sare ya 0-0. Hata hivyo kipindi cha nyongezadakika 30, pia zilitoka sare 0-0. Hata hivyo Atletico imefanikiwa kuingia hatua ya robo baada ya kupata ushindi wake kwa njia ya matuta  kwa kupaata penati 8-7 dhidi ya wapinzani wao hao..
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 450w" alt="man city" width="702" height="935" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
Moja ya matukio ya mchezo huo yalivyokuwa na hekaheka.. wakati wa wachezaji wa timu ya Man City na Dynamo
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 600w" alt="3204" width="702" height="481" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" />
Baadhi ya wachezaji wa Man City wakipunga mikono kwa mashabiki wao mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger