TRA

TRA

Monday, April 24, 2017

Mbunge wa Jimbo la Mchinga atembelea wapigakura wake

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mbunge wa Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, Hamidu Bobali akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Lichinji Kata ya Kilangala katika mkutano wa kujadili ujenzi wa shule ya awali ya Kiwalala.  


 Mbunge wa jimbo la Mchinga Hamidu Bobali akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali wa Kata ya Milola mkoani Lindi kuhusu changamoto wanazokabilia nazo walio wengi ni wafanyabiashara (PICHA NA SULEIMAN MSUYA)



Suleman Msuya, Lindi 

WAFANYABIASHARA wa Kata ya Milola Jimbo la Mchinga mkoani Lindi wameshauriwa kutumia benki kukopa na kuwa wa kweli ili kuepuka usumbufu kwa watoa mikopo.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa jimbo hilo Hamidu Bobali wakati akizungumza nao kwenye mkutano ambao ulishirikisha maofisa kutoka Benki ya NMB na Jeshi la Polisi mkoani Lindi.

Alisema amelazimika kukutana na wafanyabiashara hao ili kuweza kusikiliza kero zao hasa kuhusu mikopo na usalama na kuangalia njia ya kuzitatua.

Bobali alisema wafanyabiashara hao wanapaswa kutumia rasilimali na biashara zao kujipatia mikopo katika benki hiyo ya NMB kwani ipo kwa ajili yao.

Mbunge huyo alisema benki hiyo ndio ina uhakika kutoa huduma ya mikopo kwa asilimia 99 kutokana na kuwa chini ya serikali hivyo ni vema wafanyabiashara wakaitumia kupata mikopo.

"Si kwamba naipigia debe NMB ila huo ndio ukweli kuwa ndio benki ambayo bado ipo imara kifedha kwa asilimia 99 ila mnaweza kukopa kwingine silazimishi mtu Mimi nataka muendelee," alisema.

Alisema taswira mbaya iliyopo katika benki hiyo kuhusu wananchi wa Milola haipaswi kuwepo hivyo ni vema wakajirekebisha na kutumia fursa hiyo kwa sasa.

Bobali alisema matarajio yake ni kuona Milola kunakuwa na wafanyabiashara wa kubwa wa jumla hivyo njia muafaka ni kukopa katika benki.

Akizungumzia kuhusu asalam kwa wafanyabiashara na wananchi wa Milola alisema anatarajia kujenga kituo kikubwa cha POLISI kwa kushirikiana na wananchi, serikali na Jeshi Polisi.

Alisema matarajio yake ni kuona kasi ya kukua kwa mji huo inaendana na nyenzo zote muhimu ikiwepo kituo cha polisi .

Bobali alisema kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) inatarajia kukutana na kukubaliana utaratibu wa kujenga kituo hicho hivyo wananchi waendelee kusubiri.

Aidha, Bobali alisema atahakikisha kuwa changamoto ya ushuru ambayo wafanyabiashara wanakutana nayo inatatuliwa kwa wakati.

Aliwahaahidi wafanyabiashara hao kuwaletea wataalam kutoka halmashauri kuwasikiliza ili kufikia muafaka na kwamba wao wataendelea kujadili kwenye vikao vya halmashauri.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa nazi Hadija Abdallah alimuambia mbunge kuwa kutokana na kero ambazo wanakutana nazo kwenye biashara hiyo wanafikiria kuacha hivyo hata ushauri wa kuwataka wakope benki hauwezi kufanikiwa.

Abdallah alisema watu wa halmashauri hawataki kusikiliza kilio chao na kwamba nazi moja inakatwa ushuru wa sh.20 hali ambayo inawapatia hasara.

Alitoa ushauri kwa mbunge kuwasaidia ili biashara ya nazi ikatiwe leseni kwani si matunda.

Akizungumza katika mkutano huo Kaimu Meneja wa Mikopo NMB Lindi, Robert Pazi alisema benki hiyo ipo tayari kutoa mikopo kwa mtu yoyote ambaye atakidhi vigezo na mkweli.

Pazi alisema baadhi ya wafanyabiashara ni waongo hali ambayo imechafua hadhi ya Milola hivyo kutoa rai wabadilike ili weweze kunufaika na mkopo.

"Tunaambia ukweli hapa Milola tatizo baadhi yenu si wa kweli hivyo kama hamtabadilika hamtapata mkopo badilikeni, " alisema.

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi aliwaahidi wafanyabiashara na wananchi kuwa wapo tayari kushirikiana nao kuhakikisha kituo kinajengwa kwa wakati na haraka.

"Sisi wakati ukifika tutatoa ushauri namna ya ujenzi wa Kituo hiki hivyo jipangane tupo pamoja," alisema.








 

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger