Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura akizungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu
wanawake “Twiga Stars” alipowatembelea kambini kwa leo jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye
Nkenyenge na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi
Shang’a (kulia).
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga
akitoa shukura kwa Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia
wadhamini Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati
Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura(wapili kutoka kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo
leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la
Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu
wanawake “Twiga Stars” (Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo
jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a.
Mjumbe
wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a.
akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu wanawake “Twiga
Stars” Bibi. Nasra Juma wakati
wa ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura (hayupo pichani) kambini kwao leo jijini Dar es
Salaam.
Baadhi
ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars”
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao
leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu
ya Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika
uwanjja wa Taifa.
Picha na WHUSM.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akimweleza jambo Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund mara baada ya
kumkabidhi shilingi milioni tatu zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye
hakutaka jina lake litajwe kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya
mpira wa miguu ya Twiga Stars. Mhasibu Osmund alizipeleka fedha
hizo katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Naibu
Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
akimkabidhi Mhasibu wa wizara hiyo Godfrey Osmund shilingi milioni tatu
zilizotolewa na mdau wa michezo ambaye hakutaka jina lake litajwe
kwaajili ya kuisaidia timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Twiga Stars.
Fedha hizo zimewekwa katika Benki ya NMB Bank House akaunti namba “20110001677 inayojulikana kwa jina la Twiga Stars Special Fund”.
Picha na Anna Nkinda.
SHARE
No comments:
Post a Comment