WanaChama
cha Mapinduzi na Wananchi wakiwa pamoja wakisherehekea kuapishwa kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,pia wakiwepo
Waandishi wa Habari kushuhudia mambo mbali mbali yanayoendelea katika
zoezi la kuapishwa kwa Rais.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akifuatana na Makamanda wakati alipokuwa akikagua gwaride la Vikosi vya
Brass Band leo katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,baada ya
kuapishwa rasmi kwa kuongoza Zanzibar katika kipindi cha Pili cha Awamu
ya saba.
Viongozi
mbali mbali wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa leo katika
sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein
akitia saini hati ya kiapo mbele ya Jaji Mkuu Mhe,Omar Othman Makungu
baadanya kumalizikika kwa zoezi hilo lililofanyika leo katika Uwanja wa
Amaan Studium Mjini Unguja(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid
Yahya Mzee.
Waaandishi
wa Habari Wapigapicha wakijaribu kufanikisha kazi yao kupata matukio
mbali mbali wakati wa Sherehe za kumuapisha kwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein leo katika Uwanja
wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa
katika Uwanja wa Amaan Studium baada ya kuapishwa leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiwapungia mkono wananchi baada ya zoezi la kuapishwa pamoja na kukagua
gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lenye muundo wa ALfa
unaoashiria mwanzo wa Uongozi wake kwa kipindi cha pili katika Uwanja wa
Amaan Studium baada ya kuapishwa rasmi leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipeana mkono na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakati
aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya
kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipeana mkono na Mkuu wa KMKM Hassan MUssa Komodoo wakati
aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya
kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akipeana mkono na Kaimu Mkuu wa JKU Kanali Ali Mtumweni Hamadi wakati
aliposalimiana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama baada ya
kumalizika zoezi la kuapishwa katika Uwanja wa Amaan Studium leo.[Picha
na Ikulu.]
SHARE
No comments:
Post a Comment