TRA

TRA

Tuesday, March 15, 2016

ZIARA YA WAZIRI MKUU, MAJALIWA WILAYA YA MISSENYI MKOANI KAGERA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kiwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda kwenye Ranchi ya Missenyi mkoani Kagera Machi 14, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Uganda waishio kwenye mpakani waliovuka mpaka ili kumuona wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wialyani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
Baadhi ya wananchi wa Uganda waishio mpakani wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wilayani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. Wananchi hao wa Uganda walivuka mpaka ili kumuona Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majajaliwa akifurahia zawadi ya picha aliyozawadiwa na wananchi wa Kata ya Kakunyu wilayani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
Afisa Mifugo wa Kata ya Kakunyu wilayani Missenyi, Eric Kagoro akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu na wananchi kuhusu tuhuma kuwa analinda wafugaji toka nchi jirani wanaolisha mifugo yao kwenye ardhi ya Tanzania kinyemela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger