Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya
Matokeo ya Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka
2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Uzinduzi huo
umefanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo
wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS). Uzinduzi huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mwakilishi wa Shirika la
Kazi Duniani (ILO), Ms. Mary Kawar alipohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya
Matokeo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka
2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Uzinduzi huo
umefanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi wa serikali, wadau wa takwimu, mashirika ya umma na binafsi
pamoja na wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya
Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015
uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Uzinduzi huo umefanyika
jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akionyesha vitabu vya ripoti ya Utafiti wa
Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 wakati wa uzinduzi
wa ripoti hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Hall Jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na baadhi ya washiriki
waliohudhuria katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo
wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS). Uzinduzi huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam. (PICHA
ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Na Veronica Kazimoto
Watu
wenye umri wa miaka mitano na zaidi wanatumia asilimia 71 ya muda wao
mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji kama vile kujihudumia,
kulala na starehe.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akizindua
Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa
mwaka 2014/2015 Jijini Dar es Salaam uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS).
Waziri
Mhagama alisema Serikali ya Awamu ya Tano ilikiona kiashiria hiki cha
matumizi ya muda ndio maana iliamua kuingia madarakani na kauli mbiu ya
HAPA KAZI TU.
“Matokeo
ya utafiti huu yanaonesha watu wenye uwezo wa kufanyakazi hutumia
asilimia 71 ya muda wao kwenye shughuli zisizo za uzalishaji na asilimia
18.5 ya muda hutumika katika shughuli za uzalishaji huku asilimia 10.6
hutumika katika shughuli za nyumbani zisizokuwa na malipo” Amesema
Waziri Mhagama.
Amefafanua
kuwa nchi haiwezi kupiga hatua katika maendeleo zaidi ya kuhimiza na
kuhamasisha nguvu itumike zaidi katika uzalishaji.
Aidha,
Mhagama amesema kuwa katika utafiti huo, wanaume walitumia asilimia
23.8 ya muda wao katika uzalishaji ikilinganishwa na wanawake ambao
walitumia asilimia 13.5 katika uzalishaji na asilimia 16.5 ya muda wao
waliitumia katika shughuli za nyumbani zisizokuwa na malipo huku wanaume
wakitumia asilimia 4.4 kwa shughuli za nyumbani.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa amesema matokeo ya utafiti huu ni ya muhimu sana katika kutekeleza
mipango ya maendeleo ya wananchi hususani vijana na watoto ambao ni
Taifa la kesho.
“Ninalisemea
hili kwa kuwa utafiti huu umeonesha kuwa bado watoto wetu
wanatumikishwa katika kazi hatarishi katika maisha yao.” Amesema
Dkt.Chuwa.
Dkt.
Albina Chuwa amesema kuwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea na
juhudi za kukusanya taarifa na kutumia mifumo ya kisasa inayotumia
teknolojia kwa lengo la kupunguza gharama za kukusanya takwimu nchini.
Utafiti
huu wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi ni wa tano kufanyika tangu
Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika
mwaka 1965, 1990/91, 2000/1, 2006/7 na huu wa 2014/15.
SHARE














No comments:
Post a Comment