JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Juni,
2016 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteua
Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi.
Kufuatia
uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck
Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe.
Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake
ulitenguliwa.
Mawaziri
walioteuliwa katika mabadiliko haya wataapishwa Jumatatu tarehe 13 Juni, 2016
saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
11
Juni, 2016
SHARE
No comments:
Post a Comment