ZAIDI ya Wananchi 3,000 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Januari 29, 2018 wamefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kuitikia wito wa Mhe. Paul Makonda, kupeleka malalamiko ya kero zao zihusuzo dhulma walizofanyiwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, a,meandaa wanasheria 160, watakaopitia
nyaraka mbalimbali zitakazowasilishwa na wananchi hao, ili kuwapatia ushauri wa
kisheria.
Wananchi
hao wametaabika kwa muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao Walizochuma kwa
Tabu na sasa kupitia huduma ya Masada wa kisheria uliotangazwa na RC Makonda
wanaamni watarejeshewa haki yao.
RC
Makonda amesema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza leo inatoa picha kamili
Kuwa wapo viongozi wasiotekeleza vyema majukumu yao ya kiofisi kwenye idara zao
ambapo ameahidi kuwawajibisha.
Aidha
RC Makonda amesema kilichomgusa kuandaa Wiki ya msaada wa kisheria ni baada
kubaini uwepo wa wananchi wanaonyanyasiki na hata kufikia hatua ya kufa kwa
presha au kupooza miili baada ya kudhulumiwa na watu wenye pesa au wanaotumia
uelewa wa sheria kukandamiza wanyonge.
Kutokana
na idadi kuwa kubwa wanaoendelea kujitokeza RC Makonda anaongeza wanasheria
wengi zaidi ili kuhakikisha Kila anaefika na kupata namba anahudumiwa ipasavyo
ambapo amewaomba wanasheria kuhakikisha wanawasikiliza wananchi kwa umakini na
kuchambua nyaraka kwa ufasaha na wasitoe hukumu.
Makonda
amesema katika zoezi hili limehusisha Wanasheria wabobezi, Wataalamu wa
kutambua nyaraka zilizogushiwa, watendaji wa Ardhi na watumishi wa Mahakama
ambao wapo kwaajili ya kuwahudumia Wananchi.
RC
Makonda amesema baada ya kupokea ripoti kamili ya kesi zote atasimama
kuhakikisha Hakuna mnyonge anabaki akinyanyasika.
Zoezi
la kusikiliza wananchi waliodhulumiwa Mali zao ikiwemo Nyumba, Viwanja, Magari,
Mirathi na Kazi litaendelea hadi siku ya Ijumaa ya February 02.
Nao
wananchi waliojitokeza wamemshukuru RC Makonda kwa kutambua Tabu wanazozipata
baada ya kudhulumiwa na wajanja ambapo wengine wamesema wamepoteza Waume, Wake
zao na wengine kupata magonjwa baada ya kudhulumiwa na wametaabika Muda mrefu
kutafuta haki pasipo kufanikiwa lakini kupitia utendaji kazi makini wa RC
Makonda wanaamni haki inapatikana.
SHARE
No comments:
Post a Comment