
Barcelona, Hispania
Mshambuliaji
wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi
21 jela kutokana na kulipa kukwepa kodi, vyombo vya habari vya Hispania
vimeripoti.
Baba
yake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kifungo kwa kukwepa kulipa kodi
inayokadiriwa kufikia Euro 4.1 milioni kwa kipindi cha kuanzia 2007 hadi
2009.

Pia,
wawili hao watakumbanana na faini ya mamilioni ya Euro kwa kutumia njia
za ulipaji wa kodi wa Belize na Uruguay, ambako kuna kiwango cha chini,
zilizokuwa na lengo la kujipatia kipato cha haki za picha zake (Messi).
Hata hivyo, Messi mwenye tuzo tano za mchezaji bora wa dunia wa Fifa na baba yake wanaweza kukwepa maisha ya jela.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, kipengele cha kwenda jela chini ya miaka miwili kinaweza kutumikiwa kwa makubaliano maalumu.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, kipengele cha kwenda jela chini ya miaka miwili kinaweza kutumikiwa kwa makubaliano maalumu.
Mshambuliaji
huyo wa Barca na baba yake walikutwa na hatia ya makosa matatu katika
kodi wakati wa hukumu ya jana katika Mahakama ya Barcelona.
Wakati wa
kusikilizwa kwa kesi hiyo, Lionel Messi alisema kwamba ‘hajui chochote’
juu ya usimamizi wa fedha zake, akidai kuwa kazi yake ni ‘kucheza
mpira’.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment