
Meneja
Uendelezaji wa Masuala ya Kibiashara wa Vodacom Tanzania (Business
Continuity Management), Ajit Mistry (kushoto) na Afisa msimamizi wa
michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hamed (wa pili kushoto)
wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia)
akiwaonyesha namba ya simu ya Shomari Almasi mkazi wa Mwanza aliyeibuka
mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- katika droo ya mwezi ya
promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ inayowawezesha wateja wa mtandao huo
kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100. Jumla ya
washindi 61 wamepatikana kupitia promosheni hiyo. Ili mteja aweze
kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO” kwenda namba
15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neno ”WIN”
kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya mwezi
ya promosheni ya”Kamata Mpunga”ambapo Shomari Almasi, mkazi wa Mwanza,
aliibuka mshindi wa mwezi wa kitita cha shilingi Milioni 20/- Wengine
katika picha kushoto ni Ofisa msimamizi wa michezo ya kubahatisha
Tanzania, Abdallah Hamed na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,
Mathew Kampambe.
Mkazi wa
kitongoji cha Mkoani kilichopo Nyamagana jijini Mwanza,Shomari Almas
ameibuka mshindi mwezi wa kitita cha shilingi milioni 20 kupitia
promosheni ya ”Kamata Mpunga”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania.
Akiongea
kwa furaha baada ya kutangazwa kuwa ameibuka kuwa mshindi wa droo ya
mwezi Shomari Almasi ambaye anajishughulisha na kilimo na ufugaji
alisema kuwa ndoto yake ya kuboresha maisha yake imetimia.
“Nashukuru
Vodacom kwa kuleta promosheni hii kwa kuwa wakati nashiriki sikujua
kama nitaibuka na ushindi.Nikipatiwa fedha hizo nitaendeleza shughuli
zangu za kilimo na ufugaji pia mipango yangu ya kuoa na kuazisha familia
yangu itafanikiwa”.Alisema.
Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa promosheni hii
ambayo inaendelea imeishawezesha wateja 61 wa Vodacom kujishindia vitita
vya mamilioni ya fedha.Washindi 58 wamejinyakulia shilingi milioni 1
kila mmoja,washindi watatu wa mwezi wamejinyakulia shilingi milioni 5
kila mmoja.
“Napenda
kutoa wito kwa wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla ambao
hawajajiunga na mtandao wetu waweze kujiunga na kuchangamkia promosheni
hii kwani kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kuna washindi 3
ambapo kila mshindi anajinyakulia shilingi Milioni 1/- na kila mwisho wa
wiki yaani Jumapili kuna mshindi mmoja wa Milioni 5/= na mwisho wa
mwezi kuna mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya
mwisho wa promosheni ni ya kitita cha shilingi Milioni 100/= “Alisema
Aliongeza
kusema kuwa ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii ni rahisi
sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa
kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa
kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali
atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na
mteja atakatwa shilingi 300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”. maswali
atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na
lingine likiwa sio sahihi.
Kwa
wateja ambao hawana nafasi ya kujibu maswali ili wasipitwe na promosheni
hii alisema wanatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakatwa
kiasi cha shilingi 200 tu watakuwa hawahangaiki kujibu maswali ila
watakuwa wameingizwa kwa droo moja kwa moja.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment