
Watu sita
wameuawa nchini Kenya baada ya washambuliaji wanaoshukiwa kuwa wa kundi
la itikadi kali la Al-Shabaab kuyafyatulia risasi mabasi mawili
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Somalia.
Inspekta
Jenerali mkuu wa Polisi IGP Joseph Boinnet, amesema maafisa wa jeshi
hilo walioko kwenye eneo la tukio walikuta watu sita wakiwa wamepigwa
risasi na kuuawa, na kuongeza kuwa msako dhidi ya magaidi hao ulikuwa
unaendelea.
Boinnet
alisema watu wengine wawili wamejeruhiwa, lakini mratibu wa usalama wa
kanda ya Kaskazini-Mashariki Mohammed Saleh alisema watu wengi
walijeruhiwa. Haikubainika bado iwapo wahanga wa shambulio hilo walikuwa
raia au maafisa wa polisi waliokuwa wanatoa ulinzi katika mabasi hayo.
Shambulio
hilo la Ijumaa asubuhi limetokea karibu na El Wak katika kaunti ya
Mandera, eneo maskini la vijiji katika nchi hiyo ambako mashambulizi ya
maafa sawa na hilo katika siku za nyuma yamedaiwa na kundi la Al-Shabaab
lenye mafungamano na mtandao wa Al-Qaeda.
Kamishna
wa kaunti ya Mandera Fredrick Shisia ameliambia shirika la habari la
Reuters, kuwa shambulio hilo lilitokea majira ya saa tatu na nusu
asubuhi ya Ijumaa, wakati mabasi hayo yakisafiri kwenda mjini Mandera
kutoka mji mkuu Nairobi.
Mashambulio ya huko nyuma
Shambulio
baya zaidi lilikuwa lile la Novemba 2014, wakati washambuliaji
waliojihami kwa silaha walipolisimamisha basi na kuwatenganisha abiria
kwa msingi wa dini na kisha kuwachinja wasio Waislamu 28. Shambulio sawa
Desemba 2015 lilisababisha vifo vya watu watu, baada ya abiria Waislamu
kuwakinga wenzao Wakristu.
Kundi la
Al-Shabaab linapambana kuianguisha serikali inayoungwa mkono na jumuiya
ya kimataifa mjini Mogadishu tangu mwaka 2007, lakini sasa limegeuzia
mashambulizi yake dhidi ya Kenya, baada ya jeshi la nchi hiyo kutumwa
nchini Somalia mwaka 2011 kupambana na waasi hao wa Kiislamu.
Tangu
wakati huo Al-Shabaab imefanya mashambulizi ya mfululizo dhidi ya raia
katika maeneo tofauti ya Kenya, likiwemo jengo la maduka mjini Nairobi,
chuo kikuu cha Garrisa kaskazini-mashariki mwa nchi na vijiji vya pwani
ya nchi hiyo.
Siku ya
Alhamisi, wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilitoa onyo kwa raia wa
nchi hiyo kuepuka kusafiri katika maeneo ya mipakani mwa Kenya kwa
sababu ya vitisho vya kundi la Al-Shabaab, ambapo El Wak na Mandera ni
miongoni mwa maeneo waliotahadharishwa kuyatemebelea.
'Kenya iko salama'
Afisa
mwandamizi katika wizara ya mambo ya ndani ya Kenya alisema onyo hilo
halikuwa la haki kwa sababu ya kile alichodai kuwa usalama wa nchi hiyo
ulikuwa umerejeshwa. Afisa huyo Karanja Kibicho, alisema Kenya iko
salama, muda mfupi kabla ya habari za shambulio la sasa kujulikana.
Wiki
iliyopita maafisa watano wa polisi waliuawa katika eneo hilo katika
shambulizi ambalo pia kundi la Al-Shabaa lilinyooshewa kidole.'Kenya iko
salama'
Afisa
mwandamizi katika wizara ya mambo ya ndani ya Kenya alisema onyo hilo
halikuwa la haki kwa sababu ya kile alichodai kuwa usalama wa nchi hiyo
ulikuwa umerejeshwa. Afisa huyo Karanja Kibicho, alisema Kenya iko
salama, muda mfupi kabla ya habari za shambulio la sasa kujulikana.
Wiki
iliyopita maafisa watano wa polisi waliuawa katika eneo hilo katika
shambulizi ambalo pia kundi la Al-Shabaa lilinyooshewa kidole.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment