
Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanika jijini Mwanza.

Wakaguzi
wa magari kutoka jeshi la Polisi wakifuatilia mafunzo ya ukaguzi wa
magari kwa vitendo kutoka kwa Mkufunzi Hubert Kubo kutoka kampuni ya
CFAO wakati wa semina ya ukaguzi wa magari iliyofanyika jijini Mwanza.



Wakaguzi
wa magari kutoka jeshi la Polisi walitembelea maeneo ya kiwanda
7/8-.Wakaguzi wa magari kutoka jeshi la Polisi wakishauriana jinsi ya
ukaguzi wa magari makubwa wakati wa semina hiyo.
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Katika
mkakati wake wa kushirikiana na serikali na jamii katika kutoa elimu ya
usalama,kampuni ya TBL Group imedhamini semina kwa wakaguzi wa magari
kutoka Jeshi la Polisi jijini Mwanza ambayo imefanyika katika kiwanda
cha TBL cha Mwanza na kuendeshwa na Mtaalamu wa magari kutoka kampuni ya
CFAO,Bw.Hubert Kubo.
Semina
hiyo iliendeshwa kwa njia shirikishi ambapo washiriki walijadiliana
masuala mbalimbali yanayohusiana na usalama barabarani na changamoto
zilizopo katika kukagua vyombo vya moto na jinsi ya kupunguza ajali za
barabarani nchini.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment